Na Emanueli Ndanshau | ||
HAI |
Baada ya maafa ya Mvua kubwa na
upepo mkali iliyosababisha maafa katika maeneo mengi ya wilaya ya Hai,hali hiyo
imeanza kutumika ndivyo sivyo na baadhi ya wananchi wakitegemea kunufaika na
misaada zaidi.
Hali hiyo imekuwa ikitumiwa na
mwanamama anayefahamika kwa jina la Aziza Mohammed ambaye kutokana na taharuki
ya upepo na mvua hiyo alilazimika kukimbilia katika choo chake cha kisasa
ambacho alijenga kikiwa imara kuliko nyumba yake ya kuishi siku chache kabla ya
tukio.
Bibi Aziza Mohammed akiwa katika pozi la kawaida mara anaposikia makundi
mbalimbali yanatembelea eneo la maafa pamoja na mjukuu wake ambaye ana
matatizo ya akili |
Baada ya tufani hilo kutulia na
makundi mbalimbali ya watu wakiwemo viongozi kuanza kutembelea maeneo hayo ndipo
alipobaini kuwa kukaa kwake chooni kunaweza kumpatia misaada na kuamua kufanya
hivyo kwa kila anapopewa taarifa ya ujio wa viongozi katika eneo hilo.
Tofauti na wenzake waliopata maafa
ambao waliombewa makazi ama kukaribishwa kwa majirani,lakini kwa Bibi
Aziza ilikuwa ni patashika kukubali kuhama mpaka pale viongozi wa Kata na
Kijiji pamoja na maofisa wa Maendeleo ya Jamii walipoenda kumshawishi na
kukubali kuhama.
Hata hivyo hakuweza kuridhika hadi
baada ya kubaini kuwa atapatiwa msaada wa bati za kutosheleza vyumba viwili
ambavyo vitajengwa kwa kununuliwa tofali za kuchoma na wasamaria wema na hivyo
kukubali kurudishwa na baadhi ya waandishi wa habari ili kwenda kupigwa picha
kule chooni akichukuliwa kutoka kule alikopewa hifadhi.
Hatua hiyo ilijitokeza baada ya
kutoridhika na vyumba viwili na kuwaeleza waandishi wa habari hao kuwa mkoa na
wilaya umeshindwa kumsaidia na hivyo anamsubiri Waziri mkuu Mizengo Pinda
"Ni kweli ilikuwa ni patashika
kumwamisha huyo mama kutokana na mtazamo wake kwamba akiishi hapo chooni baada
ya nyumba yake kuezuliwa paa atapata misaada,lakini viongozi wa kitongoji,kijiji
na wa maendeleo ya jamii walimwelimisha baadaye alikubali,lakini cha ajabu,leo
waandishi wa habari hao wamemchukuwa na kumrudisha kule chooni ili kupata
picha" alisema mmoja wa viongozi wa kitongoji
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus
Makunga ameeleza kuwa serikali wilayani humo kwa kushirikiana na mbunge wa
jimbo la Hai,Freeman Mbowe wameweka mazingira ya dharura ya kusaidia kaya
ambazo makazi yao yapo katika hali mbaya yakiwemo ya Bibi Aziza na wengine
wengi kwa kutenga fedha za kununua matofali ya kuchoma.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga[Kulia] akipokea msaada wa
mabati kutoka kwa viongozi wa kiwanda cha Bonite Bottlers cha mjini
Moshi na tofali imara za kuchoma za vyumba viwili hazipo pichani |
Makunga ameeleza kuwa pamoja na
kuwepo kwa msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP
kupitia Bonite Bottlers,lakini ni vigumu kuezeka katika nyumba nyingi kutokana
na kukosa uimara ikiwemo aliyekuwa akiishi Bibi Aziza na hivyo wanajipanga
kumnunulia
Lakini pia alisema kuwa msaada kama
huo utapelekwa kwa mzee aliyemtaja kwa jina moja la mzee Omar wa kitongoji cha
kijiweni ambaye hana msaada kabisa pamoja na mama mjane wa kijiji cha Kikavu
Chini ambaye atapatiwa bati lakini kijiji kimekubali kufanya harambe ya
kumsaidia kukamilisha nyumba yake.
Makunga ameeleza kutokana na uchache
wa msaada hasa bati bado uchanganuzi unafanyika ili kuweza kuzigawa kwa wale
ambao wana hali mbaya zaidi.
Aidha Makunga amefafanua kwamba
serikali wilayani humo haijawahi kuwaleta waandishi wa habari kupiga picha
jinsi wananchi wanavyoishi bali kama ilivyo kwa majukumu ya waandishi wa habari
kufanyakazi bila ya mipaka wamekuwa wakija na wasamaria wema wanaoleta misaada
kwa lengo la kutaka kujua hali ya maafa hayo.
Nae Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mhe
Leonidas Gama,ni alikuwa miongoni mwa viongozi waliotembelea vijiji vitano vya
ukanda wa tambarare vilivyokumbwa na maafa ya mvua na upepo mkali katika wilaya
ya Hai kwa lengo la kuwafariji waliokumbwa na maafa hayo.
Mhe Gama aliwafariji wananchi wa
vijiji hivyo vya Shirimgungani,Mijongweni,Kwatito,Ngosero na Kikavu Chini.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama akizungumza na wathirika wa maafa Hai |
Mkuu huyo wa mkoa aliwahakikishia
wananchi hao kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakikisha kuwa wanajikimu
kimaisha kwa kuwa na mahitaji ya msingi ya chakula ambacho kitawapa nguvu ya
kujipanga upya kwa maisha.
Aliuagiza uongozi wa wilaya
kuangalia uwezekano wa kuwa na mbegu fupi za mahindi zinazokomaa kwa muda mfupi
ili wananchi hao ambao hivi sasa wanajiandaa kwa msimu wa kilimo wawe na
uhakika wa kupata mavuno ya kutosha.
Alisema kutokana na mazingira
yanayojitokeza ya mvua za sasa kuja kwa kasi lolote linaweza kutokea likiwemo
la mvua hizo kukata kwa muda mfupi.
Aidha Mheshimiwa Gama aliutaka
uongozi wa wilaya sasa kuwa na programu ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na
nyumba imara ili kuepukana na maafa ya kila mwaka pale zinapojitokeza mvua
kubwa zinazoambanatana na upepo
0 comments:
Post a Comment