Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo
Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na
mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu
mbalimbali wakitazama mpira.
Blog hii imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni
watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema
wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu
hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana
alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye
shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka
taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment