Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha,
Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger',
iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi
karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la
utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results
Now).
*************************************************
Akieleza malengo hayo hayo
msemaji mkuu wa wizara ya fedha, INGIAHEDI MDUMA amesema wizara ya fedha
imejipanga Kutafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8
hadi kufikia mwaka 2015/16
Pamoja na hayo Mduma
amesema pia wamedhamiria kupunguza nakisi katika bajeti ya Serikali kwa
shilingi trilioni 4 kufikia mwaka 2015/16 na Kutekeleza miradi ya PPP
yenye thamani ya shilingi trilioni 6 kufikia mwaka 2015/16
Malengo mengine ni
kuhakikisha kwamba shughuli za BRN zinapatiwa fedha za kutekeleza miradi
iliyopangwa ili kuweza kusimamia malengo yaliyokusudiwa
Aidha amesema viashiria vya
utafutaji wa mapato vinavyotekelezwa na Wizara ya Fedha vimegawanyika
katika sehemu kuu nne ikiwemo ya mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi,
ubia katika sekta ya umma na sekta binafsi na kudhibiti matumizi ya
serikali.
katika kuelezea malengo
hayo amesema Katika kipindi cha Julai – Disemba, 2013 jumla ya shilingi
bilioni 215.0 zimekusanywa kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa
kwenye maabara za BRN.
chanzo;Michuzi blog
chanzo;Michuzi blog
0 comments:
Post a Comment