MJUE MRISHO MPOTO NA HARAKATI ZAKE ZAKUPIGA VITA EBOLA NCHINI!!




Msanii Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la Mjomba 
Utunzi wa mashairi, mikogo na staili yake ya mavazi stejini inaweza kuwa chanzo cha kumfanya afananishwe na simba dume aliye barani Afrika aking’ara nchini hata katika anga za kimataifa.

Mrisho Mpoto alimaarufu kwa jina la MJOMBA anaweza kuwa mmoja kati ya wasanii wachache wa Afrika wanaofanya vizuri katika sanaa ya jukwaa, inayojumuisha muziki, maonyesho na ushereheshaji, ambao hufanyika kwa wahusika kuwasilisha uzoefu wa tukio halisi jukwaani.

Mrisho Mpoto ni mwenyeji wa Songea, mkoani Ruvuma katika Kijiji cha Namtumbo, kusini mwa Tanzania.

Mpoto ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Balozi wa Ebola amekuwa akitumia sanaa yake kufikisha ujumbe anaokusudia kwa mashabiki wake, wananchi hata katika Ikulu ya rais. Moja ya kazi za mwanzo zilizopendwa za msanii huyu ni wmbo wa; ‘Salamu Zangu’, ‘Adela, ‘Mjomba’, ‘Chocheeni Kuni’ na nyinginezo.

Katika maisha ya kawaida nje ya sanaa maishani mwake, Mpoto anaeleza kuwa amefanikiwa kukutana mara tatu na Rais Jakaya Kikwete kwa kile alichoeleza ni kutokana na ushawishi wa sanaa yake.

Mrisho anaitaja mara ya tatu kuwa ilikuwa Alhamisi wiki hii, akieleza kuwa safari hii lengo lilikuwa kuzungumzia nafasi yake ya ubalozi wa kupambana na ugonjwa wa ebola nchini.

Katika mahojiano yake anaeleza anavyotumia nafasi hiyo ya ubalozi.

Mwandishi: Kwa mara ya kwanza na ya pili ulikutana wapi na Rais Jakaya Kikwete na ulizungumza naye nini?

Mpoto: Kwa mara ya kwanza kabla ya kuonana naye Ikulu, nilikutana naye Ufaransa kwenye mashindano ya utunzi wa mashairi duniani mwaka 2009/10. Sikuwa vizuri, basi akanikaribisha Ubalozi wa Tanzania na kunisaidia sana.

 Kwa nafasi hiyo nilifarijika sana na kutambua Rais wangu ni kiongozi wa aina gani. Kama alifanya hivyo kwangu, basi ninaamini atakuwa amewasaidia wengi waliopo nje au anaokutana nao.

Kwa upande wa Ikulu, nimemtembelea mara mbili. Mwaka 2011 na mwaka 2012, ilitokea mara moja. Mazungumzo yetu mara zote yalilenga kujua tasnia ikoje, changamoto na mazingira ya sanaa yetu hapa nyumbani. Ni kiongozi anayetamani kuona wasanii tunafanikiwa, pia anaonekana kupenda sana kazi zetu.

Mwandishi: Umekuwa ukitumia muda gani kwa mazungumzo yenu unapoketi meza moja na Rais Kikwete?

Mpoto: Haa haaa, huwa natumia nusu saa, dakika 45 au vinginevyo kutegemeana na mazungumzo yetu.

Mwandishi: Kupitia nafasi hizo, umewahi kufikiri labda ni fursa ya kumaliza shida zako?
Mpoto: Hapana kaka, unajua wengi wanadhani kukutana na kiongozi kama yule basi ndiyo ubadilishe mazungumzo na kuanza kutangaza shida zako. Mimi ni mtu wa mikakati na lazima utambue kama ipo ipo tu.
Mwandishi: Huoni kama fursa hiyo inaweza kukuweka kwenye mazingira magumu kwa baadhi ya makundi kwenye jamii?
 
Mpoto: Siangalii kundi fulani linanitazama vipi, ila ninazingatia kile ninachoona kina manufaa kwa ajili yangu, tasnia na jamii yote. Siwezi kukwepa makundi yanayobeza harakati zangu. Kwa mfano, baada ya kumaliza sherehe za kukabidhiwa kwa Katiba Inayopendekezwa kule Dodoma, kuna makundi fulani yamenitukana sana kwenye mitandao, eti kwamba nimekuwa msaliti.
Sidhani kama ni sahihi, kwa sababu mimi ni msanii, Katiba hiyo imepitisha mambo mengi ya wasanii, ambayo yameungwa mkono na wasanii wote. Mambo yaliyopingwa ni masilahi ya wanasiasa kinyume na maslahi ya kazi yangu.
Kwa watu makini, watakubaliana na uamuzi wangu wa kuunga mkono harakati hizo za Katiba. Mimi sitetei masilahi ya wanasiasa, hilo lieleweke wazi.
Mwandishi: Kama unaweza kuunga mkono kwenye harakati hizo, kwenye uchaguzi mkuu ujao, CCM wakikuomba uwapigie kampeni utakubali au utakataa?
Mpoto: Sijajua kama nitakubali au nitakataa. Lakini kwa sasa msimamo wangu, nisingependa kufanya kazi za wanasiasa. Kuna vitu ambavyo ni lazima kuwa na msimamo na uheshimiwe
Mwandishi: Unadhani ni kigezo gani kimesababisha wewe uchaguliwe kuwa Balozi wa Ebora nchini na siyo watu wengine?
Mpoto: Siwezi kujua kwa kweli, lakini ninavyodhani itakuwa ni nafasi yangu tu kama msanii, muelimishaji na msanii niliye karibu zaidi na jamiii.

 Kwa nchi nyingine, uteuzi huo umefanyika kwa wacheza mpira na wanasiasa, ila hapa Bongo wameona mimi ninafaa zaidi katika harakati hizo.
 Jukumu tulilopewa katika harakati hizo ni uchangishaji wa Euro 20,000 sawa na takriban Sh42,460,000 kwa kila nchi na Rais wa nchi anatakiwa kusaini makubaliano hayo, ndiyo sababu ya kuomba kukutana na Rais wangu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment