
Mhe. Habib Mnyaa alihoji serikali inachukua hatua gani juu
ya watu wanaotuma picha zao zisizo na maadili mitandaoni zikiwemo za
kina Wema na Diamond wanazopiga wakiwa chumbani na kuweka kwenye
mitandao ya kijamii?.
Katika
majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame
Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili
zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu
serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online
Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha
hizo na kuchukua hatua madhubuti”.

Baada
ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu
juu ya picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na
binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana
wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe.
Spika kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua
zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona
ila tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka.
0 comments:
Post a Comment