Wengi tumekuwa tukitumia kama mboga
au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida
za nyanya chungu kiafya.
Pamoja na kufanya mboga kuwa na
ladha na harufu ya aina yake, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa
binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga na kuimarisha afya ya mlaji.
Nyanya chungu ipo kwenye kundi la
mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin A, B, na C ambazo zote kwa
pamoja hufanya kazi ya kuobresha afya ya mwili kwa ujumla.
Nyanya chungu pia husaidia
kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji kuepukana na magonwja ya mara kwa
mara. Hizi pia ni kinga iayoweza kumwepusha mlaji kupata maradhi ya moyo. Kwa
wagonjwa wa kisukari nyanya chungu pia ni dawa inayoweza kusaidia katika
kupunguza kiwango cha sukari ndani ya mwili.
Vitamin K inayopatikana ndani ya
nyanya chungu inasaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima
la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.
Licha ya kuwa karibu, asilimia 90 ya
nyanya chugu ni maji mboga hii pia inajumuisha madini ya chuma na potassium.
0 comments:
Post a Comment