UTATA WA KATIBA WAFIKIA KIKOMO!!



 

BUNGE Maalumu la Katiba, limepitisha marekebisho ya kanuni ili liweze kufikia hatua ya mwisho ya upigaji kura ya Katiba iliyopendekezwa kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 2, 2014.

Hatua hiyo imelenga kumaliza vikao vya Bunge hilo katika muda uliopangwa kwa mujibu wa sheria Oktoba 4 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Bunge hilo, Bw. Samuel Sitta, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu uwasilishwaji wa Azimio la kupitisha Marekebisho ya Kanuni za Bunge la Katiba.

Bw. Sitta alisema wajumbe wa Bunge hilo wasiopungua 480, wanatarajiwa kupiga kura ambapo kwa mujibu wa kanuni ambazo zilikuwepo awali kabla ya mapendekezo ya mabadiliko hayo, ingechukua siku nyingi kukamilisha kazi ya upigaji kura kupitia kifungu kwa kifungu.

"Kanuni zilivyo sasa, kama hatutafanya mabadiliko, itachukua dakika mbili kwa kila mjumbe kupiga kura kwenye kila kifungu hivyo kwa siku, tutatumia wastani wa dakika 960 kwa ibara moja.

"Tunatarajia ibara zitakuwa 300 ambazo tungehitaji siku 300 kukamilisha mchakato huu, muda huo utakuwa kinyume na utaratibu uliopangwa kwa maana ya kuipitia ibara moja kwa siku moja," alisema Bw. Sitta.

Alisisitiza kuwa, marekebisho yaliyofanyika yamelenga kuhakikisha kazi ya upigaji kura inakuwa rahisi na kumalizika katika muda uliopangwa kisheria wa siku 60.

Awali, akiwasilisha maelezo ya marekebisho ya Kanuni za Bunge hilo za mwaka 2014 kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Amon Mpanju alisema kanuni zilizofanyiwa mabadiliko ni namba 36 na 38.

Alisema marekebisho hayo yatamwezesha mjumbe aliye nje ya eneo la Bunge kwa ruhusa ya maandishi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, kupiga kura ya wazi na siri kwa njia ya nukushi na mtandao.

Aliongeza kuwa, hatua nyingine ni kumwezesha mjumbe kupiga kura katika muda usiozidi siku saba kwa urahisi na ufanisi.

Akitoa ufafanuzi wa wajumbe walioko Hijjah, Shekhe Norman Jongo, alisema mjumbe anayetekeleza ibada hiyo hakatazwi kupiga kura mradi hajafikia hatua za mwisho wa ibada.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment