Arusha.
Mpango wa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha mikoa ya Arusha na Mara utaendelea kama ilivyotangazwa na Serikali isipokuwa katika eneo la kilometa 53 lililoko katika Hifadhi ya Serengeti.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara
Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Deusdedit Kakoko alipokuwa
akizungumzia hukumu ya Mahakama ya Afrika ya Mashariki iliyozuia ujenzi
wa barabara hiyo.
“Serikali imekwishatangaza kuwa kipande cha barabara ambacho kinapita Hifadhi ya Serengeti chenye urefu ya kilomita 53 hakitajengwa kwa lami, hivyo naamini ujenzi wa maeneo mengine hautakuwa umeingilia uamuzi wa mahakama hiyo,” alisema Kakoko.

0 comments:
Post a Comment