JK ASAMEHE WAFUNGWA 3,967 WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MUUNGANO!!


Rais Jakaya Kikwete
 
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 3,967 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, alisema katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana kuwa msamaha huo umetolewa na Rais Kikwete kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Wafungwa watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni pamoja na wote waliopunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49 (1) cha sheria ya Magereza sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara 2 (i-xviii).


Wengine ni wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu (TB) na Saratani.


Wamo pia wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi, wafungwa wa kike walioingia na mimba na walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya, wafungwa wenye ugonjwa wa akili na wenye ulemavu wa mwili.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment