REAL MADRID YAANZA WIKI NGUMU BILA RONALDO, BARCA YAFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSU NEYMAR!!

WAKATI Mabingwa wa Ulaya Real Madrid Jumatano Usiku wakianza Wiki ngumu kwao katika azma yao ya kupaa kileleni mwa La Liga, Mahasimu wao Barcelona wameburutwa Mahakamani katika sakata linaloendelea la Uhamisho wa Neymar.
Jumatano Usiku, Real wako kwao Santiago Bernabeu kucheza Mechi yao ya kiporo na Sevilla ambayo haikuchezwa Mwezi Desemba kutokana na wao kuwa Nchini Morocco kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu ambalo walilitwaa.
Kwenye Mechi hii na Sevilla, Real watamkosa Supastaa wao Cristiano Ronaldo ambae atakuwa akimalizia Kifungo cha Mechi mbili baada ya kupewa Kadi Nyekundu.
Lakini Jumamosi Ronaldo atarejea kilingeni kwenye Dabi ya Jiji la Madrid huko Vicente Calderon wakati Real watakuwa Wageni wa Mahasimu zao Atletico Madrid kwenye Mechi ya La Liga.
Hivi sasa Real ndio wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 51 kwa Mechi 20 wakifuatiwa na Barca wenye Pointi 50 kwa Mechi 21 na kisha Atletico wenye Pointi 47 kwa Mechi 21 na ya 4 ni Sevilla yenye Pointi 42 kwa Mechi 20.
Wakati huo huo, Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ameburutwa Mahakamani kwa madai ya ukwepaji Kodi unaohusu Uhamisho wa Neymar kutoka Santos ya Brazil kuhamia Barcelona.
Inadaiwa Bartomeu na Klabu ya Barca ilikwepa kulipa Kodi ya Pauni Milioni 2.1 inayohusu Uhamisho wa Neymar.
Rais Bartomeu ametakiwa kutinga Mahakamani Februari 13 kwa Jaji ambae pia anasikiliza Kesi inayomhusu Rais wa zamani wa Barca, Sandro Rosell, anaedaiwa kutakatisha Fedha zinazohusu Uhamisho huo huo wa Neymar.
LA LIGA
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumatano Februari 4
2245 Real Madrid CF v Sevilla FC
Ijumaa Februari 6
2245 Deportivo La Coruna v SD Eibar
Jumamosi Februari 7
1800 Atletico de Madrid v Real Madrid CF
2000 Villarreal CF v Granada CF
2200 Levante v Malaga CF
0001 Real Sociedad v Celta de Vigo
Jumapili Februari 8
1400 Cordoba CF v UD Almeria
1900 Getafe CF v Sevilla FC
2100 RCD Espanyol v Valencia C.F
2300 Athletic Bilbao v Barcelona
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment