MENEJA MASOKO WA COCA COLA IRINGA AUWAWA KIKATILII!!!!




Watu wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani iringa ikiwemo la mmoja kupigwa risasi na mwingine kufa maji.

Akithibitisha kutokea kwa  tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani iringa Wankyo Nyigesa amesema Steven Mbwilo (40) ambaye ni afisa masoko wa kampuni ya coca cola amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kifuni  katika kijiji cha mtiri wilayani mufindi, hata ivyo baada ya kukaguliwa marehemu alikutwa na tsh 4,733,000/= na simu yake ya mkononi.
  Aidha kutoka na na tukio hilo Pascal Benedict mkazi wa tunduma (44) na Seleman Juma mkazi wa Soweto (42) wanashikiliwa na jeshi la polisi wakihusishwa na mauaji hayo.

Katika tukio lingine Aloyce Mlimakifye (60) amekutwa amekufa kwenye mto kitwao kikonde  katika kijiji cha mtitu wilaya ya kilolo na chanzo cha kifo hicho ni ulevi.

Wakati huo huo katika maeneo ya stendi ya ipogoro jeshi la polisi limewakamata Yasu Yatibu (20) na Mireto Wolklang (20) wote wakiwa ni raia wa Ethiopia wameingia  nchini bila kibali.

Kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa iringa Wankyo Nyigesa ametoa wito kwa jamii wawe wanatoa taarifa katika jeshi la polisi pindi wanapoona watu tafauti katika maeneo yao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment