Ripoti moja imebaini kwamba karibia dola millioni 14 za kugharamia vita dhidi ya ebola nchini Sierra Leone hazijulikani zilipo.
Mkaguzi huyo amesema kuwa taasisi hizo mbili zilishindwa kutoa stakhabadhi za kandarasi zilizotolewa kununua ambulansi na kujenga kituo cha matibabu ya ebola .
Ripoti hiyo imesema kulikuwa na malipo ya dharura mara mbili kwa wabunge na maafisa wa polisi na kwamba fedha zilipewa watu fulani badala ya mashirika ambayo wangewakilisha.
Hatahivyo Serikali nchini humo hajatoa jibu lolote kuhusu ripoti hiyo.
0 comments:
Post a Comment