Rais
wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt
akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
usiku huu jijini Dar es salaam.
|
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh.
Joachim Gauck na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais
wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck akiwa na mkewe Bibi Schadt na Makamu
wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakitazama vikundi
mbalimbali vya burudani wakati wa mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini
Dar es salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakiwa na nyuso za furaha.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim
Gauck na msafara wake wamewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere usiku huu majira ya saa 2.40.
Mara baada ya kuwasili uwanjani
hapo akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt amelakiwa na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali pia
mapokezi ya burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na
wananchi waliojitokeza kumpokea.
Rais huyo ambaye anaitembelea
Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Jakaya
Kikwete atapata mapokezi rasmi kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya
saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atapata fursa ya kukagua
gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania na kupigiwa mizinga 21.
Akiwa nchini Tanzania Rais Joachim
Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu
jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi
wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na
wafanyabiashara wa Dar es salaam.
Pia Februari 4, 2015, Rais huyo
ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na Rais wa
Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake
nchini Tanzania Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani
atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini
Arusha.
0 comments:
Post a Comment