MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu ifikapo leo jioni awe ametoa tangazo katika
gazeti la serikali ili kuruhusu tozo mpya za mahoteli kwenye hifadhi la
sivyo ajiuzulu cheo chake.
Zitto ameyasema hayo leo wakati akichangia kwenye majadiliano ya hoja za kamati bungeni.
Zitto amesema kuwa serikali inapoteza shilingi bilioni 2 kila mwezi
kwa kitendo cha Waziri wa Utalii kutotoa tangazo katika gazeti la
Serikali ili kuruhusu tozo mpya za mahoteli katika Hifadhi.
Tangu mwaka 2011 mpaka 2014, Serikali imepoteza tshs 80 bilioni.
0 comments:
Post a Comment