Wengi
wetu tunaifahamu nyanya kama kiungo kwenye mapishi yetu au hata kachumbari
kwenye mlo.
Hata
hivyo, watafiti nchini marekani wamebaini kuwa wanawake wanaokunywa juisi ya
nyanya angalau mara moja kwa wiki,
wanapunguza kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya matiti.
wanapunguza kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya matiti.
Kwa
mfano, wanaeleza kuwa glasi moja ya nyanya kwa siku ina kiwango sahihi na cha
kutosha cha madini ya Lycopene, ambacho ni kemikali za mimea zinazoaminika
kuondoa kukua kwa saratani.
Madini
ya lycopene ndio yanayozipa nyanya rangi yake nyekundu na nyanya hizo zimeundwa
zaidi na vichocheo vyenye uwezo wa kuzuia saratani hiyo.
Watafiti
katika chuo kikuu cha Rutgers Nchini Marekani walipima, kiwango cha vichocheo
kwa wanawake 70 wenye miaka 55 na kuendelea ambao walitumia juisi ya nyanya kwa
wiki 10. Wanawake hao ambao wengi walikuwa waneen kupita kiasi na baadhi wenye
dalili ya saratani, walipungua uzito na saratani ilikwisha.
0 comments:
Post a Comment