ALICHOKISEMA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI ZITTO KABWE MARA BAADA YAKUTANGAZWA KUVULIWA UANACHAMA!!

Mbunge wa Kigoma kaskazini Mh Zitto Zuberi Kabwe. (Picha na Maktaba)
Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho!!

Zitto Kabwe amesema
‘Mimi nilikuwa kwenye kikao cha Mamlaka ya EWURA nikajulishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kesi yetu imetupwa’
‘Lakini kwenye kumbukumbu zetu ilikuwa twende Mahakamani tarehe 12 mwezi wa 3 sio kwa ajili ya maamuzi ni kwa ajili ya kesi kutajwa, kwetu sisi tumeshangazwa kwamba kesi imefanyika leo kwa maamuzi kesi ambayo ilipaswa itajwe vile vile siku hiyo hiyo Chadema kutangaza kwamba wamenivua uanachama mimi mpaka sasa sina taarifa rasmi na naendelea na kazi zangu kama kawaida’
Kwenye sentensi nyingine Zitto Kabwe amesema; ‘leo nilikua na EWURA.. ratiba yangu inaonyesha kesho nitakuwa na TANESCo na keshokutwa nitakuwa nashughulikia mabilioni ya Uswisi’
‘Kwa upande wangu mimi taarifa yoyote rasmi sina, nitaweza kusema chochote baada ya kupata taarifa rasmi.. Wanasheria wangu wamekwenda Mahakamani kwa ajili ya kupata hiyo Judgement na kuweza kuona hatua gani zitakazofuata katika hiyo Judgement’– Zitto Kabwe.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment