Kauli hiyo ilitolewa kwenye ofisi ndogo za Bunge
Dar es Salaam wakati wa kikao cha mashauriano baina ya TR, Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Kamati hiyo kilichofanyika
jana na kukubaliana kuwa TR asimamie mchakato huo.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema: “Baada ya
majadiliano kamati inamuagiza TR asimamie mchakato huu ambao umekwisha
anza miaka miwili iliyopita kuhakikisha ifikapo Juni 30, iwe
imewasilisha ripoti yake kabla ya Bajeti ya Serikali kuleta mpango
mkakati huo.”
Zitto aliongeza kuwa, “Tunataka kuwa na shirika
jipya linaloweza kujiongoza na TR ndiye ana wajibu wa hilo, mchakato huu
ulipoanza haukuwa umesimamiwa vizuri kwani hata TR mwenyewe hakuwa
anaufahamu lakini sasa tunamkabidhi jukumu hilo yeye mwenyewe.”
Alisema mapato wanayopata Tanapa na Ngorongoro yanaweza kununua ndege na wala si kuchangia mapato kama ilivyokuwa awali.
Kwa upande wake, Mafuru alisema: “Mimi nitakwenda
kutumia taarifa za kamati ambazo zilikwisha undwa na kuangalia jinsi
gani shirika litafufuliwa pamoja na maoni ya kamati kisha nitakuja na
kile ambacho kamati imekipendekeza.”
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL), Salim Msoma alisema, suala la wawekezaji hususani wa nje
halitakiwi kutegemewa kwani linapokuja katika utekelezaji wake, miradi
yake inakuwa na changamoto nyingi.
0 comments:
Post a Comment