NEC YATHIBITISHA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUTOKUPIGA KURA.

TUME ya taifa ya Uchaguzi sasa imethibitisha kuwa wanafunzi wa Vyuo vikuu hawatapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao. 

Akizungumza katika kipindi cha kikaangoni kinachorushwa na EATV, jana Emmanuel Kawishe amesema kuwa wanafunzi hao hawataweza kupiga kura kuchagua diwani,mbunge au Rais kwa kuwa sheria inasema kila mtu atapiga kura pale alipojiandikishia.


“Sheria ya uchaguzi kifungu cha 61(3)a kuwa kila aliyejiandikisha atapiga kura alipojiandikisha” alisema Kawishe.


Aidha amefafanua kuwa vituo vyote vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1 asubuhi na vitafungwa saa kumi jioni hivyo kuwatahadharisha wapiga kura wote kuwepo kituoni kabla muda wa kufunga.


Taarifa ya kutopiga kura kwa wanafunzi wa vyuo vikuu imekuwa rasmi huku viongozi wa Wanafunzi vyuo vikuu wakihangaika kupeleka shauri mahakamani ili serikali ifungue vyuo kwa wakati na kuwapa wao fursa ya kupiga kura.


Hii ni mara ya pili kwa Vyuo vikuu kufunguliwa baada ya Oktoba, kwa mara ya kwanza ilifanyika vile vile mwaka 2010 kwa kisingizio cha mikopo ya Elimu ya juu.


Ushahidi kutoka kwa wanafunzi mbalimbali waliowahi kunufaika na mikopo wanasema serikali haijawahi kutoa mikopo kwa wakati licha ya sababu za mara kwa mara kuahirisha kufungua vyuo wakati wa Uchaguzi.


Mapema mwaka huu, Shirikisho la wanafunzi wa wanachadema wa Vyuo vikuu (Chaso) kupitia Kaimu Mratibu wao Wilfred Mwalusanya aliitaka NEC kueleza utaratibu wa kuwaandisha wanavyuo ili wakati wa kupiga kura waweze kushiriki.
Tayari tuhuma zimeanza kutolewa na wadau mbalimbali kuwa tume imetumiwa na serikali ya CCM ili kuinusuru sababu wanavyuo wamehamasika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment