Mnyika asema: Wananchi pazeni sauti tupate katiba mpya nzuri.


Mbunge wa Ubungo, John Mnyika amewaasa wananchi wa kada mbalimbali kupaza sauti zao kwa pamoja ili kulizuia Bunge lisipitishe miswada miwili ya Sheria ya Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba, kwa kuwa haitaleta katiba yenye tija kwa Taifa.

Miswada hiyo ni wa Sheria ya Marekebidho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, unalenga kumpa mamlaka Rais, kama utapishwa wa kuteua wajumbe 166 wa kuingia katika Bunge la Katiba kutoka katika makundi ya kijamii.

 Wa pili ni wa Sheria ya Kura ya Maoni wa Mwaka 2013, ambao endapo utapitishwa, utatoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) iliyopo, pamoja na mfumo wa sheria ya tume hiyo kusimamia zoezi zima la kura ya maoni. Miswada hiyo itajadiliwa katika Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ilioanza jana.

Mnyika aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kujadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba, ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Ubungo (UDI).

“Suala la Rais kuwa na mamlaka ya kuteua wabunge lilipigiwa kelele huko nyuma hadi likaondolewa, kabla ya kurudishwa tena enzi ya utawala wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa. Haifai tena kumpa Rais mamlaka ya kisheria ya kuteua wajumbe 166 toka katika makundi ya kijamaii,wa kwenda kwenye Bunge la Katiba,” alisema.

Alisema itakuwa si sahihi kupitisha muswada huo, kwa sababu watakaoteuliwa na Rais kuingia kwenye kundi hilo, watawiwa kulipa fadhila kwa aliyewateua, na hivyo kuwa upande wa serikali kwenye maamuzi ya kupitisha aina ya katiba mpya inayopendelewa na serikali.

Alisema kinachopaswa kufanyika ni kuzuia suala hilo lisitokee na badala yake, sheria ikaainisha kwa uwazi kwanza, makundi ya kijamii yanayopaswa kuwakilishwa, na ikatoa mamlaka kwa makundi hayo kuchagua yenyewe wawakilishi wao, watakaoingia kwenye idadi hiyo ya wajumbe 166, wakaounda Bunge la Katiba

     @Chadema Blog.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment