MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amezindua
mpango maalumu kwa ajili ya harambee ya kusaidia upatikanaji wa fedha
ili kusaidia kununua maabara na maktaba za kutembea katika Jimbo la
Ubungo.
Uzinduzi wa mpango huo wenye kaulimbiu
‘Uhuru dhidi ya Ujinga’ ulifanyika katika Ukumbi wa Much More, jengo la
Billicanas jijini Dar es Salaam jana.
Mnyika alieza kuwa kuanzia sasa hadi
Oktoba 14, mwaka huu, atatoa mrejesho wa pesa kiasi gani zimepatikana
kwa ajili ya kununua maabara na maktaba ya kutembea, na Desemba 9, mwaka
huu atawaita wadau mbalimbali kwa ajili ya harambee kubwa yenye lengo
ya kukusanya zaidi ya sh milioni 300.
Alisema yeye amechangia asilimia 20 ya
mshahara wake wa kila mwezi ili kampeni hiyo kupitia asasi ya maendeleo
ya Ubungo, Ubungo Development Initiative (UDI) iweze kufanikiwa, kwani
lengo ni kusaidia kupanda kwa kiwango cha elimu na ufaulu katika masomo
ya sayansi.
“Serikali itaendelea kufanya shughuli
zake kwa kutegemea kodi za wananchi lakini itachukua muda mrefu
kukamilisha huduma hizo, hivyo wadau mbalimbali wajitokeze kuunga mkono
ili kuleta ufanisi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment