Chadema kuweka hadharani maoni ya Rasimu ya Katiba mpya keshokutwa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitayaweka hadharani maoni ya wapenzi, wafuasi na wanachama wake yaliyokusanywa nchini kote, kwenye mabaraza ya katiba, keshokutwa.

Maoni hayo yalikusanywa na Chadema katika mikutano ya ndani na hadhara, kwa njia ya mtandao, simu (sms), barua pepe na maoni ya matawi ya chama hicho nje ya nchi.

Ofisa Mwandamizi wa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa maoni hayo yatawekwa hadharani baada ya kamati ndogo ya katiba ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kumaliza kuandaa ripoti yake.

Alisema ripoti hiyo itaandaliwa na CC baada ya kuyaweka maoni hayo pamoja, kabla ya kuwasilishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Tangu Agosti 12, mwaka huu, Chadema imekuwa kwenye operesheni maalum ya kukusanya maoni hayo, iliyokuwa ikifanywa na timu mbili, zikiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, kwa kutumia usafiri wa helkopta.

Kwa mujibu wa Makene, operesheni hiyo ilifanyika hadi juzi na ilifanikiwa kufika mikoa yote ya Tanzania Bara, isipokuwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

Alisema baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwenye wilaya za Tanzania Bara, viongozi wakuu wa Chadema watakwenda Zanzibar kuhitimisha mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Rasimu ya Katiba.
Pia alisema chama kinaendelea kupokea maoni kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, ambao wanaendelea kukutana katika mabaraza ya ndani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment