Nape:Madiwani wa CCM waliofukuzwa Kagera waendelee na kazi


  Sakata la kufukuzwa kwa madiwani nane wa chama cha mapinduzi(CCM)  Mkoani Kagera limechukua sura mpya baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa anayeshughulikia itikadi na uenezi Nape Nnauye kusema madiwani hao waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida na ni madiwani kisheria kutokana na kikao cha Halmashauri kuu ya Mkoa wa Kagera kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja kuwafukuzisha uwanachama madiwani hao Bwana Nape amefafanua kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa wabunge na madiwani kuwa uamuzi wa Halmashauri kuu ya Mkoa siyo wa mwisho na uamuzi huo unapaswa kupata baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe,hivyo madiwani hao ni halali mpaka kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti ambacho kitatoa maamuzi kuhusu suala hilo.
@blogger.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment