Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akiangalia
ubora wa matofali yanayotumika kujenga nyumba za wanajeshi kwa
kulivunja moja wapo ya matofari yanayofyatuliwa na Kampuni ya Shanghai
Construction Group Ltd Waziri
wa Ulinzi na JKT Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akiwa katika Kambi ya
Kigamboni kujionea ujenzi wa nyumba za wanajeshi ambazo ziko katika
hatua ya msingi Moja wapo ya ghorofa ambayo inajengwa katika kambi ya Lugalo Mafundi wakiwa kazin ni katika kambi ya Lugalo.
Katika ziara hiyo Waziri Nahodha
alianza kwa kutembelea kambi ya Kigamboni yenye nyumba 38 ambapo mpaka
sasa ujenzi upo katika hatua ya awali ya kutayarisha msingi huku
watendaji wakionesha kuwa na kasi kwani vitendea kazi vyote vinapatikana
eneo la ujenzi.
Akiwa ziarani Waziri Nahodha alihimiza ujenzi ufanyike
kwa wakati kwa kuzingatia mkataba na michoro inavyoelekeza na sio
vinginevyo. Waziri alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wakandarasi
kukiuka makubaliano ya awali ambapo aliwataka wasimamizi kutoka Wizarani
kuhakikisha kuwa mikataba na michoro inafuatwa.
Akiwa katika Kambi ya LugaloMhe.
Waziri alijionea ujenzi huo ukiwa katika hatua ya ghorofa ya pili kwa
baadhi ya nyumba na nyingine zikiwa usawa wa msingi, jambo ambalo
lilimpa matumaini makubwa kuwa kampuni hii inakamilisha ujenzi huo kwa
Kanda ya Dar es Salaam mwezi Agosti 2013.
Ujenzi huu unajumuisha kambi za
Gongolamboto, Air Wing, Kigamboni na Lugalo ambapo mradi huu unalenga
kujenga nyumba 6,064 kwa jeshi zima na ni mradi unaotarajiwa kupunguza
adha ya makazi kwa wanajeshi kuishi uraiani jambo ambalo sio utaratibu
mzuri kijeshi. Ziara ya Mhe. Nahodha pia iliambatana na Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Rose Shelukindo, baadhi ya wakuu wa Idara kutoka
Wizara ya Ulinzi na JKT na JWTZ.
Baada ya kumaliza ziara yake
alipata wasaa wa kuongea na wawakilishi wa Kampuni ya Shanghai pamoja na
usimamizi wa mradi huo na kuwataka kuwa makini katika hatua hii ya
awali kwani ndiyo hatua muhimu zaidi katika ujenzi, hususan kwa nyumba
hizo za ghorofa.
0 comments:
Post a Comment