Ujenzi wasimama uwanja wa kombe la dunia.


 
Fonte Nova
Kazi ya ujenzi katika Uwanja utakaochezewa mechi za kombe la dunia la soka mwaka 2014 nchini Brazil zimesimamishwa baada ya jaji wa mahakama kusema kuna wasiwasi kuhusu usalama.
 
Uwanja huo wa Arena da Baixada katika jiji la Curitiba ulipangiwa kuchezwa mechi nne za kombe la dunia. Ukarabati wa uwanja huo ulikwishacheleweshwa kwa kipindi kadhaa
Aliamrisha ukaguzi mpya ufanywe kabla ya kuanza tena shughuli za ujenzi. Akiongeza kusema kumegunduliwa kasoro nyingi katika ujenzi huo.
Taarifa hizo zinakuja wiki moja tu baada ya uchunguzi kufichua kwamba wafanyikazi walioajiriwa katika ujenzi wa mradi mwingine wa kombe la dunia walikabiliwa na hali ya kitumwa.
Wachunguzi hao walisema pia kwamba zaidi ya wafanyikazi 100 walioajiriwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sao Paulo wanaishi katika hali duni karibu na uwanja huo.
Mnamo mwezi wa Agosti, waziri wa michezo Aldo Rebelo alisema ana wasiwasi jinsi ujenzi ulivyochelewa katika viwanja vitano vya michuano ya kombe la dunia mwakani.
Baada ya ziara yake nchini Brazil, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke,alisema viwanja vyote lazima viwe tayari ifikapo mwezi Desemba na kuonya hatavumilia tena kuchelewesha ujenzi na hakuna 'mpango mbadala'.
Michuano ya kombe la dunia imepangwa katika viwanja 12 nchini kote Brazil.
www.info@dira yetu.blogspot.com

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment