Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa kujadili masuala muhimu ya kijinsia yanayopaswa kuingizwa katika rasimu ya Katiba mpya uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, wajumbe wa baraza hilo walitaka Katiba mpya izingatie zaidi fursa katika usawa wa uongozi na kutolea mfano kuwa kama mwanaume atakuwa waziri basi katibu mkuu awe mwanamke na siyo kupewa nafasi ya usaidizi.
"Licha ya rasimu kuainisha haki za wanawake katika ibara ya 46, lakini bado kifungu cha 1 (c) hakimpi nafasi mwanamke kushiriki kikamilifu katika chaguzi za ngazi zote za maamuzi na uongozi, hivyo kuwepo na mazingira wezeshi," alisema Mratibu wa taasisi ya wanawake ya Ulingo, Avemaria Semakafu.
Semakafu alisema katiba iweke na chombo maalum cha kusimamia haki za watoto na wanawake kwa kuwa rasimu haijaonyesha, hivyo kwa kuzingatia suala hilo utaratibu utawekwa wa kuunda tume itakayosimamia na kuhakikisha viongozi na wananchi katika ngazi zote wanaitekeleza ibara hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini (Tamwa), Valerie Msoka alisema Katiba itaje umri kamili wa mtoto na muda rasmi wa kuruhusiwa kuoa au kuolewa.
Pia alitaka itaje kiwango cha haki ya elimu kuwa mpaka kidato cha nne pamoja na kutoa mazingira rafiki ya kumwezesha watoto wa kike kupata elimu kwa usalama zaidi.
Kwa upande wake, mjumbe kutoka Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika, Matrina Kabisana alisema rasimu haijatoa haki ya kuishi kwa asilimia 100, kwani bado haijaweka kipengele cha kukataza adhabu ya kunyongwa mpaka kufa (kifo)
0 comments:
Post a Comment