MAJAMBAZI SABA WATEKA BENKI DAR ES SALAAM.

 
 

 Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M  jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa  kuwa  ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa  mpaka sasa ni kama milioni zaidi  150 zinahisiwa kuibiwa.

Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo hilo amesema  matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga vyema upya.

Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili  T220 AMV na kuondoka  nao kwa ajili ya mahojiano zaidi 

@itv

www.info@dira yetu.blogspot.com 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment