Viongozi wa Maziwa Makuu watoa siku tatu kwa M23 na Serikali ya DRC kurejea meza ya mazungumzo


 

Wapatanishi wa mgogoro wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametoa muda wa siku tatu kwa waasi wa M23 na serikali ya nchi hiyo kurejea kwenye meza ya mazungumzo huko jijini Kampala Uganda.

Hayo yamebanishwa  baada ya kikao cha viongozi wa kanda ya maziwa makuu kufanyika  huko kampala Uganda.


Kiongozi wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa amesema wao wapo tayari kwa mazungumzo wakati wowote na wajumbe wake wameshawasili mjini Kampala kwa ajili ya mazungumzo hayo.

Bertrand Bisimwa amesema kundi lake limechukua uamuzi wa kurejea katika meza ya mazungumzo wakitekeleza wito  wa mataifa yanayounda Kanda ya Maziwa Makuu kwakutaka mazungumzo kuendelea ndani ya siku tatu.

Mazungumzo hayo baina ya serikali ya DRC na kundi la waasi wa M23 yalianza tangu Desemba mwaka jana jijini Kampala lakini hadi sasa hayajafikia kwenye hatua ya kuridhisha jambo linalosababisha kuwepo na mvutano huo.

Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambaye ni mwenyekiti wa mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu amesema kuwa kuna nafasi kubwa ya makubaliano kati ya pande hizo mbili.

Mazungumzo hayo baina ya serikali ya DRC na kundi la waasi wa m23 yatakuwa chini ya mpatanishi wao Raisi wa Uganda Yoweri Museveni.

Hata hivyo wananchi wa DR Congo Wanaona kwamba mazungumzo hayo hayana tija yoyote bali suluhu ni M23 kuachana na mpango wao.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment