MICHUANO YA AFCON: IVORY COAST YAIZAMISHA CONGO DR 3-1.

Mashabiki ta timu ya Ivory Coast

Timu ya Ivory Coast imekuwa ya kwanza kutinga nusu  Fainali ya Mashindano YA Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, baada ya Jana Usiku huko Estadio de Bata, Mjini Bata, Nchini Equatorial Guinea, kuichapa Congo DR Bao 3-1.
Ivory Coast walitangulia kufunga Dakika ya 21 kwa Bao la Yaya Touré ambae aliwasha Shuti la Mita 20 na kumwacha Kipa machachari Kidiaba akitapatapa.
Congo DR walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 24 iliyotolewa baada ya Bailly kuunawa Mpira na Mbokani kufunga.
Lakini Ivory Coast walienda mbele 2-1 katika Dakika ya 41 mchezaji Gervinho aliepokea pasi ya mchezaji  Bony aliyoitumbukiza nyavuni na kuandika bao la pili kwa Ivory Coast.
Hadi Mapumziko Ivory Coast 2 Congo DR 1.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 68, Wilifried Kanon aliipa Ivory Coast Bao la 3 na kutinga Fainali kwa Bao 3-1.
Hatahivyo michuano hiyo itaendelea siku ya Alhamisi itakapokuwa Nusu Fainali nyingine kati ya Wenyeji Equatorial Guinea na Ghana.
VIKOSI:
Ivory Coast (Mfumo 4-4-2): Gbohouo; Aurier, Bailly, K. Toure, Kanon; Gradel, Serey Die, Yaya Toure, Tiene; Bony, Gervinho.
Cote D'Ivoire substitutes: Barry, Viera, Assale, Doukoure, Doumbia, Kalou, Tallo, Akpa Akpro, Diomande, Traore, Sayouba.
DR Congo (Mfumo 4-2-3-1): Kidiaba; Issama, Kimwaki, Zakuani, Kasusula; Mbemba, Makiadi; Bokila, Mabwati, Bolasie; Mbokani.
Akiba: Oualembo, Munganga, Mulumbu, Kage, Kebano, Mabele, Kabananga, Kudimbana, Mongongu, Mabidi, Mubele, Mandanda.
Refa: Neant Alioum [Cameroun]

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment