Madagascar wanapiga kura leo kumchagua Rais.


130817180254_madagascar_election_andry_rajoelina_lalao_ravalomanana_didier_ratsiraka_304x171_afpmontage_c4b47.jpg
Wananchi wa Madagascar wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo tangu yalipofanyika mapinduzi yaliyoungwa mkono na jeshi miaka minne iliyopita.
Wagombea 33 wanawania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi huo, ambao umeahirishwa mara tatu mwaka huu.

Wagombea wawili wanaopewa nafasi ya kushinda, wanaahidi kujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka ya mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 92% ya wananchi milioni 21 wa Madagascar wanaishi chini ya dola mbili kwa siku.
Rais Andry Rajoelina alimng'oa madarakani Marc Ravalomanana mwaka 2009, na kulitumbukiza taifa hilo katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kusababisha nchi hiyo kutengwa na jumuiya ya kimataifa na kunyimwa misaada kutoka nje.
Mvutano wa Kisiasa
Baada ya kupora madaraka, Bwana Rajoelina alitangaza kuwa kungekuwa na katiba mpya na uchaguzi kufanyika ndani ya miezi 24.
Mwezi Mei mwaka 2009 ilikubalika kuwa marais wote wa zamani wangeruhusiwa kugombea katika uchaguzi. Hata hivyo hilo halikufanyika mwaka 2009 au 2010.
Mwezi Januari mwaka huu Bwana Rajoelina na Bwana Ravalomanana wote walikubali kutogombea katika uchaguzi huu, ikiwa ni makubaliano na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, chombo cha kikanda ambacho Madagascar ni moja ya nchi wanachama wake.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi huu, ulipangwa kufanyika Julai 2013 lakini ukasogezwa mbele hadi mwezi Agosti kwa sababu mke wa Bwana Ravalomanana, Lalao - na baadaye Bwana Rajoelina mwenyewe kuamua kugombea, hali iliyosababisha nchi wahisani kusitisha fedha kwa ajili ya uchaguzi huo.
Bwana Rajoelina na Lalao Ravalomanana walizuiwa kugombea na mahakama ya uchaguzi pia ilimwondoa katika orodha ya wagombea, rais wa zamani Didier Ratsiraka baada ya wote watatu kukataa kujiondoa.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment