SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, TFF, Jumapili Oktoba 27, litafanya Uchaguzi Mkuu Jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa NSSF Waterfront ambapo litachagua Viongozi wake wakuu huku nafasi ya Rais ikigombewa na Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily Malinzi.
Kikao ambacho kitafanya Uchaguzi huo ni Mkutano Mkuu wa TFF ambao pia utahudhuriwa Mwakilishi kutoka FIFA, Ashford Mamelodi ambae ni Ofisa Maendeleo wa Kanda, Magdi Shams El Din ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar, ZFA.
Nae Rais wa TFF anaemaliza muda wake, Leodegar Tenga, amesemaamefurahishwa na jinsi kampeni za uchaguzi zinavyoendeshwa na hasa jinsi Wagombea walivyokuwa wakielezea kile wanachotaka kuufanyia Mpira wa Miguu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF hapo Jana, Tenga, ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF, amesema: “Ombi langu ni kwamba kampeni zimeanza vizuri, Watu wanazungumza hoja zaidi. Ni jukumu la Wajumbe kupima na kufanya uamuzi. Kwangu mimi nimejitayarisha kumkabidhi Katiba, Rais mpya wa TFF.”
Tenga, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati, CECAFA, amesema kazi kubwa iliyofanywa na uongozi wake ni kujenga Taasisi (TFF) pamoja na kuweka Mifumo (Structure) inayoainisha majukumu ya kila mmoja.
“Ajenda yetu wakati tunaingia madarakani mwaka 2005 ilikuwa ni kujenga Taasisi. Tayari Taasisi ipo, sasa mtazamo uwe kuushughulia Mpira wa Miguu wenyewe!”
WAGOMBEA TFF:
-RAIS: Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily Malinzi
-MAKAMU WA RAIS: Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace Karia
-WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI:
-Kanda namba 1- Geita na Kagera:
Kalilo Samson
-Kanda namba 2- Mara na Mwanza:
Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Lufano
-Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu:
Epaphra Swai na Mbasha Matutu
-Kanda namba 4- Arusha na Manyara:
Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali
-Kanda namba 5- Kigoma na Tabora:
Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo
-Kanda namba 6- Katavi na Rukwa:
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo
-Kanda namba 7- Iringa na Mbeya:
Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala
-Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma:
James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge
-Kanda namba 9- Lindi na Mtwara:
Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder
-Kanda namba 10- Dodoma na Singida:
Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima, Charles Komba
-Kanda namba 11- Morogoro na Pwani:
Farid Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na Twahil Twaha Njoki
-Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani:
Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed
-Kanda namba 13- Dar es Salaam:
Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary Isack Abdulkadir
POSTED BY:www.info@dirayetu.blospot.com
0 comments:
Post a Comment