Rais Yoweri Museveni ametia saini muswaada wa sheria dhidi ya ushoga na usagaji. Hatua hiyo ya Museveni inakaidi miito iliyotolewa na wafadhili kutoka nchi za Magharibi akiwemo Rais Obama.
Sheria hiyo mpya itamaanisha mtu yoyote atakayekutwa na hatia ya
kushiriki katika vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja atakamatwa
na kushatakiwa akikabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela. Aidha
sheria hiyo inapiga marufuku harakati zozote za kuunga mkono au
kutangaza vitendo vya ushoga na ikiwa mtu atashindwa kuripoti visa
vinavyohusisha vitendo hivyo vya ushoga pia atakabiliwa na sheria.
Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amezungumza na shirika la habari Reuters na kusema kwamba rais Museveni atatia saini muswaada huo leo wakati wowote kutoka sasa. Hata hivyo sauti zinaendelea kusikika ndani ya Uganda kupinga hatuwa ya kusaini muswaada huo ambao bila shaka unaitia wasiwasi jamii hiyo.
Wanaharakati wamkosoa Museveni
"Umoja ni kitu ambacho sisi Waganda tumekuwa nacho toka zamani. Tumekuwa jamii ya kuvumiliana na kwangu ni kitu cha kusikitisha kwamba tunachagua kitu tunachotaka kubakia nacho," amesema Onziema. "Sheria ya Uingereza tunayoitumia kwa sasa Uingereza yenyewe haijaitaja kama uhalifu. Kwa nini tusifuate hilo kama tunajikita kwa Uingereza?"
Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa serikali Ofwono Opondo rais Museveni anataka kusaini muswaada huo mchana huu mbele ya umma wa mashahidi kutoka vyombo vyote vya habari vya Kimataifa ili kuuonyesha ulimwengu kwamba Uganda ni nchi huru na haiwezi kuzisujudia nchi za magharibi na wala kutishwa na mashinikizo na uchokozi wa mataifa hayo.
Waafrika wengi wapinga ushoga
Kimsingi barani Afrika ni watu wachache wanaoweza kujitokeza na kujitangaza kuwa mashoga kutokana na hali ya kuokhofia kupata mkong'oto, kufungwa na hata kutimuliwa kazini.
Kufuatia hali hiyo jamii ya mashoga na wasagaji pamoja na mashirika ya kuwatetea wanahofia sheria hiyo dhidi mashoga nchini uganda huenda ikasambaa nje ya mipaka ya taifa hilo na kuigwa katika nchi nyinginezo barani humo ambako jamii nyingi zinafuata misingi ya kidini na kuuangalia ushoga kuwa sio kitu cha kawaida.
Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amezungumza na shirika la habari Reuters na kusema kwamba rais Museveni atatia saini muswaada huo leo wakati wowote kutoka sasa. Hata hivyo sauti zinaendelea kusikika ndani ya Uganda kupinga hatuwa ya kusaini muswaada huo ambao bila shaka unaitia wasiwasi jamii hiyo.
Wanaharakati wamkosoa Museveni
Waandamanaji wakitetea haki za mashoga mjini Kampala, Uganda.
Mkurugenzi anayehusika na jinsia za waliowachache nchini humo
Pepe Onziema amepaaza sauti akimtaka rais Museveni kutafakari upya
mtazamo wake hasa akizingatia Uganda imekuwa nchi inayoridhia jamii
mbali mbali kuishi pamoja kwa amani."Umoja ni kitu ambacho sisi Waganda tumekuwa nacho toka zamani. Tumekuwa jamii ya kuvumiliana na kwangu ni kitu cha kusikitisha kwamba tunachagua kitu tunachotaka kubakia nacho," amesema Onziema. "Sheria ya Uingereza tunayoitumia kwa sasa Uingereza yenyewe haijaitaja kama uhalifu. Kwa nini tusifuate hilo kama tunajikita kwa Uingereza?"
Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa serikali Ofwono Opondo rais Museveni anataka kusaini muswaada huo mchana huu mbele ya umma wa mashahidi kutoka vyombo vyote vya habari vya Kimataifa ili kuuonyesha ulimwengu kwamba Uganda ni nchi huru na haiwezi kuzisujudia nchi za magharibi na wala kutishwa na mashinikizo na uchokozi wa mataifa hayo.
Waafrika wengi wapinga ushoga
Rais Yoweri Museveni wa Uganda anaungwa mkono na Waafrika wengi
Vitendo vya kufanya mapenzi kati ya watu wa jinsia moja ni
hatua isiyokubalika katika nchi takriban zote barani Afrika na ni tabia
iliyopigwa marufuku katika nchi 37 ikiwemo nchini Uganda ambako makundi
ya kutetea haki za Mashoga yanasema watu hao tayari wanakabiliwa na
kitisho cha kufungwa jela.Kimsingi barani Afrika ni watu wachache wanaoweza kujitokeza na kujitangaza kuwa mashoga kutokana na hali ya kuokhofia kupata mkong'oto, kufungwa na hata kutimuliwa kazini.
Kufuatia hali hiyo jamii ya mashoga na wasagaji pamoja na mashirika ya kuwatetea wanahofia sheria hiyo dhidi mashoga nchini uganda huenda ikasambaa nje ya mipaka ya taifa hilo na kuigwa katika nchi nyinginezo barani humo ambako jamii nyingi zinafuata misingi ya kidini na kuuangalia ushoga kuwa sio kitu cha kawaida.
0 comments:
Post a Comment