WAKILI BINAFSI AAPISHA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA SEGEREA!!


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Migombani-Segera, Japhet Albert Kembo akiapishwa leo jijini Dar es Salam. 

 Baada ya kusubiri kwa muda wa wiki mbili ili wajumbe wa serikali ya mtaa wa Migombani-Segerea waapishwe na mamlaka husika bila mafanikio, wananchi wameamua kuwaapisha viongozi hao kwa kutumia wakili binafsi.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi katika ofisi za Serikali za Mtaa zilizopo Segerea Mwisho ambalo lilijumuisha kuapishwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Japhet Albert Kembo pamoja na wajumbe watatu ambao ni Rose Benard Mhagama, Nyangeto Flora Justin na Ramadhan Rashid Seif.
Akizungumza baada ya kuapishwa, mwenyekiti mpya wa mtaa huo amesema kuwa wananchi wamechoshwa na danadana wanazopigwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za kutowaapisha viongozi waliowachagua ndiyo maana wamefikia hatua hiyo ili kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
“Wananchi wanahitaji huduma kutoka kwa watu wanaowaamini lakini wanakosa imani pale uongozi wa manispaa unaposhindwa kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria. Wamemtafuta wakili ambaye amekuja kulisimamia suala hili kisheria na ndiyo maana zoezi limefanywa hadharani,” alisema Kembo.
Wananchi waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa hawaelewi kinachoendelea kwakuwa uchaguzi ulifanyika kama kawaida pasipo dosari yoyote na matokeo yakatangwazwa huku nafasi zote zikichukuliwa na wagombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
“Uchaguzi wetu haukuwa na matatizo na ni miongoni mwa mitaa iliyotangaza matokeo muda mfupi baada ya uchaguzi kufanyika lakini jambo la kushangaza ni kwamba viongozi wote waliochaguliwa hawajaapishwa kama ilivyofanyika kwa wengine katika manispaa hii wakati hakuna pingamizi lolote mahakamani linalozuia uhalali wa waliochaguliwa,” alisema John Kandeo, mmoja wa wananchi walioshuhudia kuapishwa kwa viongozi hao.
Akifafanua kuhusu matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 14, mwaka jana, Kembo alisema kuwa walikuwa wagombea watatu katika nafasi ya uenyekiti ambao ni yeye mwenyewe aliyepata jumla ya kura 547, Uyeka Idd wa CCM  aliyepata kura 273 na Erick Mchata wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 205.
Zoezililivyokuwa
Muda wa saa 05:00 asubuhi, wakili wa kujitegemea kutoka kampuni ya mawakili ya Ame and Company, Idd Msawanga aliwasili katika ofisi za mtaa huo na kupokelewa kwa kelele nyingi za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipaza sauti zao kwa sauti kubwa za ‘Peoples…Power.’
Wakili Msawanga alianza kwa kumuapisha mwenyekiti, peke yake, na baadaye wajumbe hao watatu kwa pamoja na kuelezwa kuwa wajumbe wawili hawakuwepo kutokana na matatizo ya kifamilia.
“Sheria ya uchaguzi inaruhusu kufanya hivi na hata hao wajumbe wawili ambao hawapo kwa leo watakaporudi nitawaapisha…ni suala la kutaarifiana tu,” alisema Msawanga.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment