UN:Mateso tele katika magereza ya Libya

misrata_torture_304x171_ap_nocredit_5e6ff.jpg
Mateso na dhuluma ambazo wakati mwingine zinasababisha vifo, zimeripotiwa kutokea sana katika magereza nchini Libya. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo inasema kuwa mateso ndio hufanyika sana baada ya mtu kukamatwa na katika siku ya kwanza ya kuhojiwa.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu 8,000 wangali wanazuiliwa kuhusiana na mgogoro wa kisiasa uliotokea mwaka 2011 ambapo aliyekuwa rais Kanali Muamar Gaddafi aliuawa.
Wengi wanazuiliwa bila ya hata kufuata mfumo wa sheria.
Kwa mujibu wa ripoti ya UN, mateso yanatumika kama njia ya kupata ukweli kutoka kwa washukiwa.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Libya kinasema kuwa kimepata taarifa za vifo vya watu 27 wakiwa wamezuiliwa tangu mwaka 2011 na kwamba sababu ya kutokea vifo ni kuwa watu hao waliteswa.
Ripoti hiyo hata hivyo, haionyeshi ikiwa mateso yanafanyika licha ya juhudi za maafisa wa utawala nchini Libya kusema kuwa yataisha na kuhakikisha mfumo sawa wa sheria unatumika.
Inaonyesha kuwa sababu kubwa ya kuwatesa watu wanaozuiliwa ni kipindi kirefu ambacho wanazuiliwa na kuhojiwa mikononi mwa makundi ya watu waliojihami.
Inapandekeza kuwa watu waliokamatwa wawe wanakabidhiwa kwa polisi.
Serikali ya Libya inakabiliwa na wakati mgumu kupambana na makundi ya watu waliojihami tangu kutokea kifo cha kanali Gaddafi mwaka 2011.
www.info@dira yetu.blogspot.com 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment