VIJANA WATAKIWA KUACHA KUKAA VIJIWENI NA KULAUMU BADALA YAKE WATUMIE FURSA ZA UJASIRIAMALI ZILIZOPO

pix2
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Bw. ELISANTE OLE GABRIELakifufungua warsha Jijini Arusha.


Vijana hapa nchini wametakiwa kuacha kukaa vijiweni na kulaumu serikali wakati hawatumii fursa mbalimbali ikiwemo fursa ya ujasiriamali na fursa nyinginezo kwa manufaa ya maisha yao ya baadae.
 
Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Elisante Ole Gabriel wakati alipokuwa akifungua maonyesho ya ujasiriamali kwa wahitimu wa stahahada ya uzamili wa masuala ya ujasiriamali kwenye chuo cha ESAMI kilichopo jijini hapa.

Ole Gabriel alisema kuwa serekali imetenga jumla y ash 6.1 bilion kwa ajili ya kuwawezesha vijana watakao ibua miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla na kuwataka vjana kutumia fursa hizo kwa manufaa yao ya baadae ilikutimiza ndoto zao.
 
‘’Hapa mmejionea ndoto mbali mbali za vijana hawa ambao wakitoka hapa teyari ni wajasiriamali wakubwa kwani maonyesho kama haya yanakuza vijana kuweza kujiajiri na kuondokana na fikra za kuajiriwa na viomba vyuo mbali mbali hapa nchini kuanza kuiga mfano wa chu hiki cha ESAMI kwani haya ndiyo mawazo serekali inayataka’’alisema ole Gabriel.
 
Nae Makamu mkuu wa chuo hicho Joseph Mumba alisema kuwa vyou na taasisi kwenye nchi nyingi za Afrika vimekuwa vikianda vijana kuingia kwenye soko la kuajiriwa na kuacha kuwapatia uwezo vijana wetu kuweza kujiajiri hapa maendeleo yetu yatabaki kuwa yakusuasua na hakuna wakumlaumu kwenye hili.
 
Mumba pia alisema ukipita mitaani utakutana na vijana wakiwa kwenye maeneo mbalimbali bila ya ajira huku wakiwa na uwezo na elimu ya kutosha hapa tatizo ni maandalizi ya vijana hawa kuwapa elimu ya kuwawezesha kujiajiri.
 
Aidha mkurugenzi wa kitengo hicho cha ujasiriamali chuoni hapo Leon Malisa alisema kuwa maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza chuoni hapo na kuwa wengi wa wanafunzi wa stahada ya uzamili ngio wanaoonyesha maonyesho hayo kwa vitendo jinsi walivyoyapokea mafunzo yao.
 
Malisa alisema kuwa mafunzo ya ujasiriamali ya maonyesho yatakuwa yakifanyika kila mwaka kwa wanafunzi kuonyesha jinsi walivyoyapokea mafunzo hayo.

@Mahmoud Ahmad -Arusha
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment