Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua
rasmi mkutano wa Mtando wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika
(ACRAN) leo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano
Afrika (ACRAN) leo jijini Dar es Salaam
…………………………………………………………………………………………………
Na Frank Shija – WHVUM
Wadau
wa sekta ya Utangazaji barani Afrika wametakiwa kulinda na kuthamini
maudhui ya ndani badala ya kukumbatia madhui ya nchi za magahari.
Rai
hiyo imetolea na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua
mkutano wa Mtandao wa Mamalaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN)
leo jijini Dar es Salaam.
Profesa
Elisante amesema ni faraja kubwa kuona kuwa wadau wa sekta ya udhibiti
mawasiliana wanashirikiana katika kutatua na kusimamia sekta hiyo muhimu
kwa pamoja kwa kuwa hiyo italeta nguvu na hari ya kusimamia maadili ya
kiafrika kwa sauti moja.
“Nafarijika
sana kuona mnavyo shirikiana katika kuhakikisha maudhui katika sekta ya
utangazaji hayaleti athari katika maadili yetu, hivyo ni seme tu
Serikali itazidi kushirikiana nanyi katika kusimamia hilo”. Alisema
Prof. Elisante.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Mamlaka za Mawasiliana Afrika
(ACRAN) Mhandishi Margaret Munyagi amesema kuwa pamoja na sekta hiyo
kulazimika kuhamia katika mfumo wa Dijiti bada Mamlaka za Udhibiti wa
Mawasiliano zinaendelea kuhakikisha kuwa hakuna mwanya kwa mahudhi
yanayokihuka maadili.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa kutoka na ushirikiano waliona wameweza kusimamia
kwa karibu misindi na maudhi ya utandazaji ili kulinda maadili ya
Mwaafrika.
“Tokea
tuhamie mfumo wa Dijiti kumekuwa na ongezeko la masafa ya utangaziji
lakini hili halijaathiri udhibiti wa maudhui kwa kuwa tumejipanga
kikamilifu na tunashirikiana vizuri kuhakikisha maadili ya mwaafrika
yanalindwa”. Alisema Mhandisi Munyagi.
Mkutano
huu wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika unafanyika
ikiwa ni mara ya pili Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu, ambapo
miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na
namana Tanzania ilivyopiga hatua katika kuhamia mfumo wa Dijiti.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment