WAZIRI
Mkuu Mizengo Pinda ametoa wito kwa vyuo vikuu , taasisi za serikali,
benki na jamii kutumia Tovuti Kuu ya Serikali na Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano katika kupata huduma mbalimbali za serikali ili
kurahisisha mawasiliano kwa gharama nafuu.
Kauli
hiyo imetolewa jana jioni na Waziri Mkuu, mheshimiwa Pinda wakati
akizindua Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius K. Nyerere jijini Dares Salaam mara baada ya kutembelea ofisi
ya Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na Mkongo wa Taifa.
Akizungumzia
kuhusu tovuti hiyo Waziri Mkuu Pinda alisema kitu muhimu ambacho mtu
yoyote kuweza kupata taarifa anazozihitaji mfano vile masuala ya kilimo
au kuomba uraia wa Tanzania. Hivyo lengo lake ni kuisadia Serikali
kufanya kazi kiutalaam.
“
Kwa hiyo ni mambo yanayoifanya nchi kwenda kwa wakati. Tumeanzisha
matumizi ya tovuti hii kwa sababu mahitaji yake katika soko ni
makubwa,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Akizungumzia
kuhusu mkongo huo alisema moja ya changamoto iliyopo matumizi yake
bado ni madogo, kwani yako chini ya asilimia tano , hivyo kuna
umuhimu wa kuongeza kasi ya matumizi.
Alisema Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto za kiusalama katika masuala hayo.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Celina Kombani aliwataka wanafunzi na vijana kubadili mtazamo kwa
kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyofaa badala yake watumie
tovuti hiyo ili kuweza kuelewa historia ya nchi ,sheria na mambo
mengine mbalimbali.
Aliongeza kuwa tovuti hiyo inarahisisha utoaji wa huduma za Serikali kwa wananchi , pia na kuongeza uwajibikaji.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Dk. Jabiri Bakari alisema
ina sehemu sita ambazo ni wananchi, Serikali,Taifaletu, Biashara, Sekta
muhimu na Mambo ya Nje.
Aliishauri Serikali kuviwezesha vitengo vya mawasiliano vya Serikali ili kuviwezesha kuweka taarifa sahihi kwa wakati.
Aidha
Jabiri alisema katika wameshaanza kazi ya kuwezesha taarifa muhimu za
Serikali kupatikana kwa njia ya simu na iko kwenye hatua nzuri.
Alizipongeza
Ofisi mbalimbali zilizowesha uwepo wa tovuti hiyo, ambazo Ofisi ya Rais
, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi, Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari –MAELEZO
na Kamati ya Bunge ya Sheria ,Katiba na Utawala.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment