| Watanzania
 wamehimizwa kutumia mayai ya ndege aina ya kwale na nyama yake kwa kuwa
 ni chakula bora chenye virutubisho mbalimbali. 
 
 
Ushauri
 huo ulitolewa na mfugaji wa kwale ambaye ni mkazi wa Tegeta, Dar es 
Salaam, Susan Magibo alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa makala hii. 
 
 
Magibo
 alisema ndege hao hivi sasa ni gumzo hapa nchini, kwani inasadikiwa 
kuwa ni dawa ya magonjwa mbalimbali kama pumu, shinikizo la damu, 
kisukari na mengineyo. 
  
 
Vile
 vile, alisema ndege hao pia wanaongeza kipato kwa kasi kwa kuwa watu wameanza 
kuelewa umuhimu wa ndege hao, hivyo kulingana na umri wao huuzwa kuanzia
 Sh 3,000 hadi 30,000 kwa ndege mmoja. 
  
 
“Mayai ya ndege hawa ni mazuri sana yakiliwa hasa yakiwa mabichi. Yana virutubisho vingi sana, hivyo yakipikwa vinapungua. 
  
 
“Kwenye
 mayai hayo kuna madini ya zink, Omega 3 ambayo yanapatikana kwenye 
mafuta ya samaki, vitamin B Complex, vitamin A na D na virutubisho vingi
 mbalimbali,” alisema Magibo. 
  
 
Aliongeza kuwa mayai hayo, pia ni aina ya chakula chenye alkaline, ambayo ni kinga tosha ya tatizo la kansa. 
  
 
“Chembechembe za kansa haziwezi kukua kwenye alkaline, hivyo ni vyema watu wote watambue umuhimu wa mayai ya ndege hawa,”alisema mfugaji huyo. 
  
 
Alisema mtandao wa http://www.quailfarm.co.uk, unaonesha jinsi ya utumiaji wa mayai hayo ili kupata matokeo mazuri kiafya. 
 
Alisema
 mtandao huo unaonesha kuwa mayai hayo, yakitumiwa kama dawa siku ya 
kwanza na ya pili mtumiaji anapaswa kula mayai matatu, siku ya tatu 
mayai manne, na siku ya tano mayai matano. 
  
 
Aliiomba
 wizara husika ya mifugo na uvuvi, kushirikiana na wafugaji hao ili 
kutoa elimu kwa Watanzania waweze kutambua umuhimu wa ndege hao, tofauti
 na inavyotafsiriwa kuwa ni ndege wa porini. | 
0 comments:
Post a Comment