Katika kuhakikisha kunakuwepo na damu ya kutosha katika benki ya damu mahospitalini waandishi wa habari wametakiwa kuwa msitari wa mbele kuchangia damu pamoja na kuwafichua wale wote wanaohusika kuuza damu kwa wagonjwa.
Wito huo umebainishwa na mtaalamu wa Mpango wa Taifa wa kuchangia damu salama Bw.George Chambo alipoongea na wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika zoezi lililofanyika la uchangiaji wa damu.
Aidha alizitaja sifa zinazotakiwa kuwa nazo mtu kabla yakutolewa damu kuwa ni pamoja na mchangiaji lazima awe na Afya njema,asiwe na magonjwa sugu,awe mtu mwenye huruma,mwenye uzito usiopungua kilo hamsini, pamoja na wingi wa damu aliokuwa nao mwilini
Vilevile Bw. Chambo alisema kuwa zipofaidi za uchangiaji wa damu katika Benki ya
damu kuwa ni pamoja na kujitambua kiafya ikiwepo kujua hali ya virusi vya ukimwi,kaswende pamoja na homa ya kifua kikuu.
Bwana Chambo amesema kuwa mpango wa kuchangia damu salama nchini
tanzania niwa hiari na unamtaka kila mwenye sifa kuchangia damu katika
benki ili kila mwenye uhitaji wakiwemo mama wajawazito, watoto chini
ya miaka mitano,wanaopata ajali kupata huduma hiyo bure.
Hatahivyo aliendelea kusema kuwa kumekuwepo na tuhuma mbali mbali
zinazowaandama madaktari na wauguzi kuhusika katika uuzaji wa damu kwa
wagonjwa bilakujali uhaba uliopo katika benki hiyo bila kujali utu,wa
mtu na huruma ya kibinadamu.
Pia Bw.Chambo alisema kuwa zipo changamoto nyingi wanazopitia ikiwepo mwitikio mdogo kwa wananchi hii ikionyosha kuwa ipo haja wananchi kupatiwa elimu juu ya umuhimu wakuchangia damu katika benki zilizopo mahospitalini.
Kwa habari picha hizi hapa!!!
|
Wataalamu kutoka Mpango wa Taifa waUchangiaji Damu salama wakiwa kwenye ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha(AJTC) mara baada ya kukaribishwa. |
|
Mtaalamu kutoka tume ya uchangiaji damu salama Nchini Bw.George Chambo akitoa utambulisho mfupi wa msafara aliofuatana nao. |
|
Wanafunzi wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazaji katika ngazi tofauti za kimasomo ikiwepo ile ya Stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji na cheti Pamoja na wanaosomea Taaluma ya Ualimu wakisikiliza umuhimu wa uchangiaji damu salama. |
|
Bwana George Chambo akijibu maswali kutoka kwa wanafunzi mara baada ya kuelezea umuhimu wa kuchangia damu salama, pamoja na sifa anazotakiwa kuwa nazo mchangiaji |
|
Wanafunzi wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazaji katika ngazi
tofauti za kimasomo ikiwepo ile ya Stashahada ya Uandishi wa Habari na
Utangazaji na cheti Pamoja na wanaosomea Taaluma ya Ualimu wakipata utaratibu utakaotumika kwenye zoezi la uchangiaji damu salama. |
|
Mwanafunzi wa ngazi ya cheti katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Yusuph Mbata akingaliwa kundi la damu alilokuwa nalo kabla ya kuchangia damu salama. |
|
Bw.Yusuph Mbata akipata ushauri nasaa pamoja na kupima msukumo wa Damu kutoka kwa Bw.Robert Shughuru ambaye ni mmoja kati ya wataalalamu kutoka Mpango wa Taifa wa Uchangiaji Damu Salama. |
|
Mtaalam kutoka mpango wa Uchangiaji Damu Salama Bw.George Chambo akichukua damu kutoka kwa mchangiaji wa kwanza katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha Bw.Yusuph Mbata. |
|
Mwanafunzi wa Taaluma ya Ualimu katika Chuo cha Uandishi na Utangazaji Arusha akiwa mapumzikoni mara baada ya kuchangia Damu |
|
Mtaalam kutoka mpango wa Uchangiaji Damu Salama Bi.Merigoreth Laswai
akichukua damu kutoka kwa mchangiaji damu kwa Bi.Elizabeth Betha katika Chuo cha Uandishi
wa Habari na Utangazaji Arusha. |
|
Mhadhiri katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha Bw.Onesmo Eliya Mbise |
|
Mhadhiri wa Chuo cha Uandishi na Utangazaji Arusha Madame Jackline Joeli akiwa mapumzikoni mara baada ya kuchangia Damu |
|
Mwanafunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ngazi ya Stashahada Bi. Regina Revocatus akipata mapumziko ya muda mara baada ya kuchangia Damu
Habari na Picha kwahisani ya Emanuel Onesmo Ndanshau
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment