BAADA kupokea vichapo viwili mfumulizo Uwanjani Emirates toka kwa Borussia Dortmund kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Chelsea kwenye CAPITAL ONE CUP, Arsenal waliibuka kwa kuitwanga Liverpool 2-0 kwenye Ligi Kuu England lakini Chelsea walijikuta wakipigwa 2-0 na Newcastle na hilo kuibua hasira na wasiwasi kwa Meneja wao Jose Mourinho.
ARSENAL POINTI 5 KILELENI LIGI KUU ENGLAND
Arsenal waliichapa Liverpool Bao 2-0 kwenye Ligi na kuongeza pengo lao kwenye uongozi wa Ligi kuwa Pointi 5.
Wakitoka kupokea vichapo viwili mfululizo Uwanjani Emirates toka kwa Borussia Dortmund kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Chelsea kwenye CAPITAL ONE CUP na kuanza Jumamosi wakiwa Pointi 2 kileleni, ushindi kwa Liverpool umewafanya wawe Pointi 5 juu hasa kwa vile wapinzani wao waliokuwa wakiwafukuza, Chelsea na Liverpool, wote kufungwa.
Mara baada ushindi huo, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, alisema: “Ilikuwa ni muhimu kushinda na kuwaonyesha Watu tunaweza kushinda Mechi kubwa.”
Aliongeza: “Difensi yetu ilisimama imara na kuwasimamisha Daniel Sturridge, Luis Suarez, Steven Gerrard na Philippe Coutinho, wanastahili sifa!”
Mechi zinazofuata kwa Arsenal ni safari ya Jumatano kwenda huko Germany kurudiana na Borussia Dortmund kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Jumapili kwenda Old Tarafford kucheza na Mabingwa wa England Manchester United kwenye Mechi ya Ligi.
KIPIGO KWA CHELSEA: MOURINHO ACHUKIZWA, WASIWASI JUU!!
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amesema amekasirika na ana wasiwasi baada ya kuchapwa Bao 2-0 na Newcastle Jumamosi Uwanja wa St James' Park kwenye Mechi ya Ligi.
Bao za Yoan Gouffran na Loic Remy ziliwapa ushindi Newcastle na kuipa kipigo cha pili Chelsea Msimu huu kwenye Ligi.
Mourinho amewaka: “Nilifanya makosa 11. Ningechagua Wachezaji wengine 11 na si hawa! Nimekasirika kwa sababu sielewi kwa nini tumefungwa. Nilitegemea kufungwa Gemu wakati Wapinzani wako moto na sisi tumekosa bahati au tumepigana kiume!”
Kipigo hicho kinamaanisha Chelsea wameambua Pointi 5 tu katika Mechi 5 za Ugenini za Ligi lakini huko kwao Stamford Bridge wamezoa Pointi 15 kati ya 15 zilizokuwepo.
Mourinho amekiri hali hii ya Chelsea inampa wasiwasi.
MOYES ACHEKELEA!
Baada Jumamosi kuichapa Fulham huko Craven Cottage Bao 3-1, Meneja wa Manchester United, David Moyes, amesema Timu yake imeanza kudhihirisha kuwa wanao uwezo wa kutetea Taji lao la Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Tangu mwanzo mwa Msimu, Wadau wengi wamekuwa wakihoji kulikoni baada ya Sir Alex Fergusom kustaafu na Timu kuanza Msimu mpya vibaya kwenye Ligi na kujikuta wako Pointi 8 nyuma ya Vinara Arsenal huku Mechi zimechezwa 10.
Lakini ushindi dhidi ya Fulham ni ushindi wao wa 4 mfululizo katika Mechi zote na wa pili mfululizo kwenye Ligi kitu ambacho walikuwa hawajakifanya chini ya Moyes.
Moyes amesema: “Tulijua ni lazima tuzoe Pointi na nilikuwa najiamini kwa hilo. Kazi yetu ni kupanda juu kwenye Msimamo wa Ligi na nina haki mwishoni mwa Msimu tutakuwa juu.”
Ushindi huo wa Bao 3-1 dhidi ya Fulham ulikuja kwa Bao za Antonio Valencia, Robin van Persie na Wayne Rooney zilizofungwa ndani ya Dakika 13 za Kipindi cha Kwanza.
Hata hivyo, kwenye Mechi hiyo, Man United walilazimika kuwatoa Tom Cleverley, Jonny Evans na Rafael wakati wa Mapumziko baada ya kuumia na hali hiyo ilipunguza makali ya Timu kwa Kipindi cha Pili.
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
GD
|
PTS
|
1
|
Arsenal
|
10
|
13
|
25
|
2
|
Chelsea
|
10
|
8
|
20
|
3
|
Liverpool
|
10
|
7
|
20
|
4
|
Man City
|
10
|
17
|
19
|
5
|
Southampton
|
10
|
7
|
19
|
6
|
Tottenham
|
9
|
4
|
19
|
7
|
Everton
|
9
|
4
|
18
|
8
|
Man Utd
|
10
|
4
|
17
|
9
|
Newcastle
|
10
|
-2
|
14
|
10
|
Hull
|
10
|
-2
|
14
|
11
|
West Brom
|
10
|
0
|
13
|
12
|
Swansea
|
9
|
1
|
11
|
13
|
Aston Villa
|
10
|
-3
|
11
|
14
|
West Ham
|
10
|
0
|
10
|
15
|
Fulham
|
10
|
-5
|
10
|
16
|
Stoke
|
10
|
-4
|
9
|
17
|
Cardiff
|
9
|
-5
|
9
|
18
|
Norwich
|
10
|
-14
|
8
|
19
|
Sunderland
|
10
|
-15
|
4
|
20
|
Crystal Palace
|
10
|
-15
|
3
|
0 comments:
Post a Comment