Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka 
wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa 
kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa 
jumuiya za kimataifa.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mkutano wa 
Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita,
 ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga amani ndani ya 
nchi.
Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.
“Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana na vitendo
 vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga amani 
nchini,” alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson 
Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza 
ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo watalifikisha suala hilo 
mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya malalamiko yao.
Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na alihoji 
kwanini awatake WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala ya 
kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo ni
 polisi na majeshi na mahakama nasrakimaro1994@gmail.com
0 comments:
Post a Comment