Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, Noel Chocha,akikagua gwaride la kikosi cha FFU katika kuadhimisha siku ya sheria nchini |
Mahakimu na Mawakili wa serikali pamoja na watumishi wa mahakama wakimsikiliza jaji |
Waalikwa mbali mbali walikuwepo katika siku ya sheria nchini |
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, Noel Chocha, akihutubia waalikwa katika siku ya sheria nchini |
Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro akitoa neno la shukrani katika siku ya sheria nchini |
Msajili wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Aaron Lyamuya, akitoa taarifa fupi ya maadhimisho ya siku ya sheria nchini |
Shekh wa mkoa Mbeya Mohamed Ally akisoma dua |
Askofu mkuu wa EAGT Mwaisabila |
Askofu Samson Mwalyego |
Kwaya ya Baby TOT ikitumbuiza ukumbini |
Kwaya ya mahakama |
IMEELEZWA kuwa Tamaa ya baadhi ya
viongozi ya kujiingiza katika kila eneo ni kiini na sababu ya vurugu
zinazotokea kila wakati baina ya watendaji na wananchi, hivyo kuhatarisha hali
ya usalama wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, Noel Chocha, wakati akizungumza katika maadhimisho
ya Sherehe za Siku ya Sheria Nchini zilizofanyika jana kimkoa katika Ukumbi wa
Mahakama kuu kanda ya Mbeya.
Jaji Chocha alisema baadhi ya Viongozi
wamekuwa wakijiingiza katika maeneo ambayo siyo taaluma yao hivyo kukosa
ufanisi wa kutatua baadhi ya changamoto ambazo hupelekea kupatikana kwa maamuzi
mabaya yanayosababisha vurugu katika jamii kwa kukosa Weredi wa jambo husika.
Alisema Ibara ya 107A(1)(2)(b) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya
utoaji wa haki katika Jamhuri itakuwa ni Mahakama na katika kutoa uamuzi wa
mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria Mahakama ndizo zinaweza
kufuata kanuni,na ndiyo msingi wa mgawanyo wa madaraka.
Alisema wapo viongozi wanaokiuka maagizo
ya mgawanyo wa madaraka ambapo kwa mujibu wa katiba Mtawala anatakiwa kubaki na
jukumu la utawala na Mbunge abaki katika majukumu kadri kadri yanavyoainishwa
kupitia ibara ya 63 na 64.
Jaji Chocha alitolea mfano mauaji
yaliyotokea wakati wa Operesheni ya Tokomeza ujangiri kuwa ilitokana na baadhi
ya viongozi kushika mambo mawili kwa wakati mmoja ingawa nia ya zoezi hilo
lilikuwa jema kutokana na wananchi wengi kutofurahishwa na vitendo vya ujangiri
ambapo aliwataka viongozi kuwa makini wakati wa kuratibu mikakati ya
kukabiliana na ufisadi kwa kutumia Sheria vizuri.
Aliongeza kuwa vita dhidi ya ujangili
iwe ya kitaifa kwa kuwahusisha wananchi wote na kwamba vita hiyo inaweza
kudhibitiwa kwa kukomesha wimbi la uhamiaji haramu ambao asilimia kubwa
wanaonekana kufadhiliwa na nchi kubwa ambazo raia wake wanajihusisha moja kwa
moja na biashara za usafirishaji wa Nyara za Serikali hususani meno na pembe za
ndovu.
Kwa upande wake Msajili wa Mahakama kuu
kanda ya Mbeya, Aaron Lyamuya, Alisema Mahakama imejipanga kuendana na mfumo wa
matokeo makubwa sasa(BRN) kwa kujiwekea mikakati mbali mbali inayoendana na
kauli mbiu isemayo ‘‘utendaji haki kwa wakati” ambapo Mwaka uliopita Mahakama
kuu iliweza kupokea Kesi 429 lakini ilisikiliza na kutoa uamuzi kwa kesi 575
hivyo kuzidi idadi ya kesi ilizopokea.
Alisema katika kipindi cha Mwaka huu
mpya ulioanza jana Mahakama kuu kanda ya Mbeya imepanga kusikiliza na kutolea
uamuzi kesi walizopokea ambazo ni 670 ingawa kuna changamoto kubwa ya upungufu
wa majaji, ambapo hadi sasa Kanda ya Mbeya ina majaji wawili mpaka sasa na
kuomba Serikali kuwaongeza ili kuendana na kasi ya kumaliza kesi kwa wakati.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro ambaye alikuwa Mgeni wa Heshima katika sherehe hizo aliipongeza
Mahakama kwa kumaliza kesi kwa wakati na kuongeza kuwa Wananchi wanapaswa kuwa
na imani na mahakama ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima.
Alisema Haki si lazima ipatikane
Mahakamani bali zianzie kwenye jamii jambo ambalo pia litasaidia kupunguza
mlundikano wa kesi na kujichukulia sheria mikononi baada ya washtakiwa
kupelekwa mahakamani na kuachiwa kutokana na maamuzi ya Mahakama lakini
kutokana na kutoamini maamuzi hayo hujichulia sheria Mkononi kwa kuamua
vinginevyo.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
|
0 comments:
Post a Comment