Kulingana
na kanuni hiyo, upande wa wanaume, pia imeainisha vazi rasmi kwa jinsia
hiyo kuwa ni suti ya Kimagharibi, shati na tai, suruali ya aina yoyote
isipokuwa suruali aina ya ‘jeans’.
Wajumbe
wanawake wa Bunge Maalumu la Katiba na wageni wa jinsi hiyo watakaovaa
nguo fupi ‘vimini’ au nguo za kubana, hawataruhusiwa kuingia ndani ya
Ukumbi wa Bunge.
Hayo
yamo katika mapendekezo ya rasimu ya kanuni za uendeshaji wa Bunge
hilo, zilizowasilishwa katika semina mahsusi ya kupokea rasimu hizo,
iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati Maalumu, Profesa Costa Mahalu.
Kanuni
ya 82 (9) ya mapendekezo hayo imeainisha vazi rasmi linaloruhusiwa kuwa
ni vazi lolote la heshima ambalo siyo la kubana mwili, lisiloonyesha
maungo.
Pia
imeainisha mavazi yanayoruhusiwa kwa wanawake kuwa ni pamoja na gauni
la kitenge au blauzi inayovaliwa na kitenge au sketi ya rangi yoyote,
suti ya kike, vazi linalovaliwa wakati wa eda na kilemba cha kadri au
mtandio.
Kwa
upande wa wanaume, mavazi rasmi ni suti ya Kiafrika au safari ya mikono
mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na fulana.
Kulingana
na kanuni hiyo, upande wa wanaume, pia imeainisha vazi rasmi kwa jinsia
hiyo kuwa ni suti ya Kimagharibi, shati na tai, suruali ya aina yoyote
isipokuwa suruali aina ya ‘jeans’.
Sehemu
ya 6 ya kanuni hiyo, imeweka wazi kuwa mjumbe yeyote wa Bunge Maalumu,
anaweza kutoa taarifa kwenye Bunge au kwenye kamati iwapo mjumbe
mwingine ataingia akiwa amevaa vazi linalovunja au kukiuka masharti ya
kanuni.
“Mwenyekiti
wa Bunge Maalum au mwenyekiti wa kamati maalumu atakaporidhika kuwa
mjumbe huyo aliyetolewa taarifa hajavaa vazi rasmi, atamwamuru atoke nje
ya ukumbi wa mikutano wa kamati,” inaseme sehemu ya kanuni hizo.
Kwa
mujibu wa kanuni hiyo, mjumbe aliyeamriwa kutoka nje ya ukumbi,
hataruhusiwa kuingia tena hadi pale atakapokwa amevaa mavazi rasmi.
Wakati huohuo, kamati hiyo imependekeza Bunge hilo liwe na kamati 16.
Akiwasilisha
taarifa ya kamati hiyo jana katika semina ya wajumbe wa Bunge hilo,
Mwenyekiti wake, Profesa Costa Mahalu, alizitaja kamati hizo kuwa ni
Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu.
Zingine; Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Kamati ya Uandishi, Kamati ya Maridhiano na Kamati nyingine 12.
|
0 comments:
Post a Comment