Wataalamu wa
kilimo pamoja na Madiwani katika wilaya ya Hai wametakiwa kufundisha wakulima
kutumia mbegu za muda mfupi pamoja na kuotesha kwakutumia matuta.
Hayo yalisemwa
na Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai Bw.Clement Zablon Kwayu wakati
alipokuwa akifungua kikao cha baraza la Halmashauri ya Hai Mkoani Kilimanjaro.
Bwana Kwayu
alisema ni vema wakulima wakahamasishwa kutumia na kuotesha mbegu za muda mfupi
ili waweze kupata chakula chakutosha kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivi
sasa.
Aidha aliendelea
kusema kuwa upo umuhimu wakuwafundisha wakulima kutumia kilimo chakuotesha kwa
matuta kutokana kunyesha mvua kubwa kwa muda mfupi na kuhamisha udongo na
mbegu.
Vile vile
amesema wenye matrecta wanalima kwakulenga kupata pesa hivyo ni vizuri wakulima
wakashauriwa na kupewa umuhimu
wakubadilisha mwelekeo wakulima mashamba tofauti na wanavyolima kila mwaka.
‘’kilimo kinachotumiwa na wenye matrecta siyo
cha kitaalamu ndiyo maana inaponyesha mvua kidogo udongo na mbegu
vinahamishwa’’ alisema Bwana Kwayu.
Hata hivyo Bwana
Kwayu aliendelea kusema kuwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa inayosababisha
mvua kupungua ni vizuri wakulima wakapewa utaalamu wakuvuna maji ya mvua kwa
matumizi ya baadae kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Kikao hicho
cha baraza la Halmashauri ya Wilaya kilikutana kujadili mambo mbalimbali
yakiwepo mgogoro wa ardhi za wananchi miatatu kumi na saba zilizochukuliwa
mwaka elfu moja mia tisa na sabini na tano kwaajili yakupanua na kujenga makao
makuu ya wilaya pia kupisha rasmu ya katiba ya halmashauri hiyo.
Chanzo:Emanuel O.Ndanshau
0 comments:
Post a Comment