Majaji wa Shindano la Kusaka la Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama
Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo wakati wa Zoezi la kusaka
vipaji vya uigizaji kuingia Hatua ya pili kwa washiriki waliofanikiwa
kupita kwenye mchujo.Kulia ni Single Mtambalike (Rich Rich), Ivon Chery
(Monalisa) na Roy Sarungi.
Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili wakifanyiwa usaili kwaajili ya hatua ya pili sasa
Muongozaji wa
Mradi wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo
kama Tanzania Movie Talents, Bw Stanford Kihole (kulia) akitoa maelekezo
kwa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili katika mashindano ya
kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania likiwa limeaingia hatua ya pili
Mkoani Mwanza
Baadhi ya
Washiriki waliofanikiwa Kuingia katika Hatua ya Pili ya Shindano la
Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie
Talents wakiwa makini kusikiliza maelekezo juu ya hatua ya pili
waliofanikiwa kuingia.
Baadhi ya
washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili wakiwa mbele ya majaji
kwaajili ya kupewa maelekezo ambapo washiriki watapewa muswada (script)
kwaajili ya hatua ya pili ambapo wataingia wawili wawili na kuanza
kuonyesha vipaji vyao.
Kikosi Kazi
kikiendelea kurekodi matukio yanayoendelea katika Shindano la Kusaka
Vipaji Vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents
linaloendelea kufanyika Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza.
Baadhi
ya washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili katika Mashindano ya
Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie
Talents wakiwa makini katika kupitia muswada (script) waliopewa na
majaji ili waweze kusoma na baadae kuingia mbele ya majaji na kuonyesha
vipaji vyao kutokana na muswada (script) waliopewa.
0 comments:
Post a Comment