Mabomba yaliathirika baada ya mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa
wiki eneo la Jangwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akiwa
na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala (wa kwanza kushoto)
walipotembelea eneo la Jangwani kkuangaliaa mabomba yalioathirika na mvua.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko akipata maelekezo
kutoka kwa Mhandisi ya namna ya kukarabati mabomba yaliyokatika eneo la
Jangwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko akiwa katika
masikitiko makubwa mara baada ya kujionea athari kubwa ya kukatika kwa
mabomba iliyotokea Jangwani baada ya mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko leo ametembelea eneo
la Jangwani, Darajani, barabara ya Morogoro kujionea uharibifu mkubwa wa
mabomba ya maji.
Mabomba hayo ya inchi 16 yenye urefu wa mita 12 yamezolewa na maji kutokana
na athari iliyoletwa na mvua kubwa ya mwishoni mwa wiki inayoendelea jijini Dar
es Salaam.
“Ni athari kubwa ambayo imesababishwa na mvua hii na mpaka kukata mabomba
ya maji, ni muda mrefu tangu mvua ya aina huu kutokea Dar es Salaam”, alisema
Inj. Mrindoko.
“Nimekuja kuangalia hali halisi na kuona namna gani tutafanya kufanya ukarabati
wa mabomba haya, ili kurudisha huduma ya maji kwa maeneo yaliyoathirika
baada ya tukio hili. Tumefanya tathmini na kuona nini cha kufanya na utekelezaji
utaanza mara moja”, aliongeza Inj. Mrindoko.
Uharibifu huu umeleta athari kwa maeneo ya Muhimbili, TBL, Mchikichini,
Upanga na Kariakoo na katikati ya Jiji kukosa maji.
Maeneo mengine yaliyoathirika ni Mtoni kwenye mtambo wa maji, ambapo
pampu za kusukuma maji kwenye chanzo cha maji zimefunikwa na maji.
Pia, Mtambo wa Ruvu Juu, Mlandizi kipande cha bomba la inchi 4 la kupoza
pampu za maji ghafi cha urefu wa mita 18 kimekatika.
Hii imesababisha maeneo ya Temeke, Tandika, Mtoni, Kurasini, Wailes na
Mbagala wanaohudumiwa na mtambo huo kukosa huduma, kutokana na
uzalishaji kusimama.
Vile vile, mfumo wa kupooza pampu za kusukuma maji ghafi kuathirika hivyo
kukosekana kwa uzalishaji tangu jana saa 11.30 jioni.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu aliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO,
Jackson Midala, Inj. Pascal Hamuli wa Wizara ya Maji na wataalamu wengine
kutoka DAWASA na kampuni za Uhandisi.
0 comments:
Post a Comment