Rais 
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed 
Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya CCM 
Kisiwandui leo katika hitma na dua ya Rais wa kwanza wa Zanzibar 
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Mke wa
 Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akitia ubani wakati wa hitma ya 
kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani 
Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini 
Unguja,wengine pia ni wake wa Viongozi.
Miongoni
 mwa wake wa Viongozi wa Zanzibar walioshiriki katika hitma ya kumuombea
 dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani 
Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini 
Unguja,akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Salma Salmin 
(kushoto).
Mabalozi
 wadogo wa Nchi mbali mbali wanaofanyia kazi Zanzibar walijumuika na 
viongozi na wananchi katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa 
Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi 
wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Wajukuu
 wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,(wa 
kwanza na watatu kushoto) wakiwa katika hitma ya kumuombea dua Rais wa 
kwanza iliyosomwa leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini 
Unguja.
Viongozi
 na wananchi wa Zanzibar waliohudhuria katika hitma ya kumuombea dua 
Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa 
leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais 
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 wakisalimiana wajukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani 
Karume,na Viongozi wakati wa hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa 
Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo mchana.
Kadhi 
Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia 
ubani kuongoza wakati Hitma na Dua ya kumuombea Rais wa kwanza wa 
Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM 
kisiwandui Mjini Unguja,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi 
Zanzibar Pandu Ameir Kificho.
Rais 
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed 
Shein,(katikati) akiungana na Viongozi,Wananchi katika kumuombe dua kwa 
Kisomo cha Hitma iliyosomwa leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini 
Zanzibar,wakiwemo Rais wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais 
mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi,Rais mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid 
Karume,Makamo wa Rais wa Tanzania Dk.Bilali,Makamo wa Pili wa Rais wa 
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine (wa pili kushoto).
Rais 
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed 
Shein,akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa
 Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,wakati wa hitma na dua iliyoombwa na 
wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo 
mchana










0 comments:
Post a Comment