MAMILIONI YA PESA YANAITAJIKA KUISADIA SUDAN:UMOJA WA MATAIFA!!

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashirika ya utoaji misaada yanahitajia dola milioni 995 kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu nchini Sudan.

Mratibu wa Misaada ya Kibindamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ali al Za'atari amesema kuwa, dola milioni 995 zinahitajika kwa ajili ya kuwasaidia karibu watu milioni 6 na laki moja nchini Sudan mwaka huu.

Afisa huyo wa UN ameashiria umuhimu wa nchi wafadhili katika kufanikisha suala hilo  na kusisitiza udharura wa kushirikiana taasisi za kimataifa na serikali ya Khartoum ili kusaidia wananchi wanaohitajia misaada. 


 Ameongeza kuwa, hali ya kibinadamu katika eneo la Darfur na Kordofan Kusini inazidi kuwa mbaya huku idadi kubwa ya wakimbizi wa Sudan Kusini pia wakivuka mpaka na kuingia katika eneo la kusini mwa Sudan.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment