Serikali
imewapongeza wahisani wa maendeleo kwa kufadhili na kukuza sanaa ambao
wamekuwa wachangiaji muhimu wa kuendeleza na kukuza uchumi na kupunguza
umasikini miongoni mwa wasanii na Taifa kwa ujumla.
Pongezi
hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bi. Sihaba Nkinga alipokuwa akizindua programu ya “kujenga
fursa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho iliyoratibiwa na asasi isiyo ya
Kiserikali ijulikanayo kwa jina la Nafasi Arts space hivi karibuni
jijini Dar es Salaam.
Sihaba
amesema kuwa kuanzishwa kwa dhana ya Programu hii kunatoa fursa ya
kujipatia kipato na kuongeza ujuzi ambao utapanua wigo wa ubunifu kwa
wasanii na kuongeza mahusiano baina yao na wasanii wengine, ikiwemo
kupanua soko la bidhaa zao.
“Nachukua
fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza kwa dhati Nafasi Art Space kwa
uamuzi huu mahususi mlioufanya wa kuratibu uanzishwaji wa Programu ya
kuibua fursa kwa wasanii wa Sanaa za Maonyesho Tanzania.” Alisema Bi.
Sihaba
Aidha
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa
sanaa imekuwa ikifanya juhudi za kutosha kuinua viwango vya sanaa nchini
kwa kuanzisha programu za kitaifa na kimataifa.
Aidha
Bi. Sihaba alisema kuwa programu kama hizi zitasaidia kubadilishana
habari, ujuzi, mikakati na ubunifu miongoni mwa wasanii kitaifa na
kimataifa.
0 comments:
Post a Comment