UUZWAJI WA MAZAO YA WAKULIMA BILA KUTUMIA VIPIMO SAHIHI BADO NI TATIZO MKOANI MBEYA!!

Baadhi ya wakulima wa viazi wakiwa wamejaza LUMBESA zao hakika mkulima anaibiwa anajiona je wahusika wa vipimo mpo?

Usipojaza RUMBESA sinunui kwako hapo sasa mweee mkulima apeleke kilio chake wapi? wahusika mpo tu maofisini 


Hii ndiyo hali halisi ya RUMBESA


Rungwe nako hivyo hivyo



Mkulima akisubiri kuuza ndizi zake wa walanguzi






Licha ya Serikali kupiga marufuku uuzwaji wa mazao ya wakulima bila kutumia vipimo sahihi bado tatizo hilo limeendelea kuota mizizi katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya.

Baadhi ya wakulima wanaoathiriwa na hali hiyo ni pamoja na wakulima wa viazi,ndizi,mahindi,ufuta,mpunga,karanga,karoti na nyanya mazao ambayo hupimwa kwa kutumia bakuli(ndonya) au debe na mara nyingine kujazwa katika magunia(RUMBESA).

Hali imekuwa na mbaya kwa wakulima hao kutokana na kutokuwa na Asasi ya kuwatetea na wafanya biashara na wachuuzi kutumia fursa hiyo kuwafuata mashambani na kuwalipa ujira mdogo na wengine kuwadhulumu wakidai watawalipa pindi mazao yatakapofika Sokoni.

Baadhi ya Wafanya biashara kutoka Mikoa mbalimbali wameanza kuingia Mkoani Mbeya na kuwarubuni wakulima kwa kununua mazao yao mashambani mwao na wao kupata faida mara tatu kwa kisingizio cha ukosefu wa usafiri.

Wakulima wa viazi wa Kata ya Itewe ni miongoni mwa wakulima waliokumbwa na dhahama hii ambapo kina mama ndiyo wamekuwa wahanga wakubwa kutokana na ukosefu wa pembejeo wamejikuta wamegeuka watumwa kwa kulipwa shilingi elfu mbili tu kwa kuvuna gunia moja la viazi.

Wameomba Benki mbalimbali nchini kuwakopesha wanawake pembejeo za kilimo kwani wao ndio wafanyaji kazi wakubwa sahambani na wao ndiyo hutunza familia na wanao uwezo wa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati.

Ombi limetolewa na wakulima hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa mamlaka za vipimo waache kukaa ofisini bali waende mashambani ambako wakilima ndiko hupata athari kubwa za kiuchumi.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro alipiga marufuku vipimo vya Debe na kuanza kutumia mizani hali iliyowafanya wakulima wa zao la ufuta kunufaika zaidi.

Juhudi hizo pia zimekuwa zikipiganiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe kwa zao la ndizi na kahawa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Michael Kadege akipiga marufuku uuzwaji wa kahawa mbichi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment