WAHAMIAJI HARAMU 47 WATIWA MBARONI KILIMANJARO

 

 

 

 

IDARA ya uhamiaji mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani humo, inawashikilia wahamiaji haramu 47 raia wa nchini Ethiopia, kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

Mbali na wahamiaji haramu hao pia idara hiyo inamshikiliwa mtu mmoja Raia wa hapa nchini , Benjamini Saimon (28) mkazi wa Kibamba Jijini Dar es salam, kwa tuhuma za kuhusika na kuwasafirisha wahamiaji haramu hao .

Akitoa taari kwa waandishi wa habari  jana ofisini kwake  mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Bw.Johannes Msumule, alisema wahamiaji hao walikamatwa April Tatu  majira ya saa tatu na Nusu  usiku katika eneo la Chekereni kata ya Kahe wilaya ya Moshi barabara kuu ya Moshi/Tanga .

Kwa mujibu wa mkuu wa uhamiaji mkoa wa  Kilimanjaro,raia hao wa Ethiopia walikamatwa wakiwa kwenye gari  lenye nambari za usajili T216 ASU aina ya Fuso, wakiwa kwenye harakati za kutaka kusafiri kwenda Afrika kusini.


Kulingana na taarifa ya Msumule ni kwamba, wahamiaji haramu hao walikamtwa na askari  pamoja na maafisa wa uhamiaji waliokuwa doria katika eneo hilo, kufuatia taarifa ilizotolewa na Raia wema za uwepo wa watu hao abao walikuwa safarini kuelekea Afrika Kusini.

Alisema kwa sasa idara ya uhamiaji imejipanga vizuri ili kuweza kutokomeza tatizo la wahamiaji haramu, ambapo kwa sasa wameanza kufuatilia ili kuwabaini watu ambao wamekuwa wakijihusisha na kazi ya kuwasafirisha wahamiaji haramu.

Alisema katika kipindi cha miezi Mitatu ya Mwaka huu Jumla ya wahamiaji haramu 216 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema mbali na watu hao jumla ya Kesi 12 zilifikishwa mahakamani ambapo moja imemalizika huku nyingine 11 zikiendelea.

Aidha Msumule alitumia pia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na idara ya uhamiaji na jeshi la polisi katika kuwabaini wahusika wa usafirishaji binadamu ili kufanikisha jitihada za serikali za  kutokomeza biashara hiyo haramu hapa nchini.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment